Pata taarifa kuu
LIBYA-QATAR

Kiongozi Mpya wa Libya aomba majeshi ya NATO yasalie hadi mwisho wa 2011

Kiongozi wa Libya Mustafa Abdel Jalil ameyataka Majeshi ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO kuendelea na kampeni yake nchini humo hadi mwishoni mwa mwaka 2011 kwa lengo la kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Jalil ameitoa kwenye Mkutano wa Nchi Marafiki wa Libya ambao unaendelea nchini Qatar katika Mji wa Doha kwa ajili ya kutafakari mustakabali mpya wa nchi hiyo baada ya kutangazwa kwa ukombozi wa nchi hiyo siku ya jumapili.

Kiongozi huyo wa Libya amesema kuwa ana matumaini kampeni hiyo itaendelea ili kuweza kuisaidia serikali yake ya Baraza la Mapito la Taifa NTC ambalo linajukumu la kurejesha demokrasia baada ya kifo cha Kanali Muammar Gaddafi.

Kauli hiyo ya Jalil imeenda sambamba na uamuzi wa NATO kuchelewa kukatisha operesheni yao ambayo imetekelezwa nchini Libya na sasa siku ya ijumaa ndiyo kutatolewa uamuzi wa mwisho ni lini Majeshi hayo yataondoka.

Msemaji wa NATO Oana Lungescu amesema washirika waliofanikisha operesheni ya kiuangushwa utawala wa Kanali Gaddafi watakutana siku ya ijumaa kutoa uamuzi wa kuendelea na kampeni yao au la.

Lungescu amesema kwa sasa kinachofanyika ni mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa NATO Andres Fogh Rasmussen, Umoja wa Mataifa UN na Viongozi wa Baraza la Mpito la Taifa NTC kuamua mustakabali wa kampeni hiyo.

Mapema Waziri wa Fedha wa Libya Ali Tarhuni alishatoa ombi kwa NATO kutaka kuendelea na kampeni yao baada ya kufanikisha kuangushwa kwa Kanali Gaddafi ambaye alizikwa usiku wa jana katika jangwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.