Pata taarifa kuu
Liberia-Yemen

Ellen Johnson Sirleaf ni miongoni mwa wanawake 3 waliotunukiwa tuzo la amani la Nobel 2011

Tuzo la Nobel la Amani mwaka 2011 imetolewa kwa wanawake watatu kwa pamoja ikiwa ni Ellen Johnson Sirleaf rais wa Liberia, Leymah Gbowee, mwanaharakati wa kuandaa harakati za amani nchini Liberia"Women of Liberia Mass Action for Peace" na Tawakkul Karman, mwanzilishi mwanaharakati nchini Yemeni muanzilishi mwaka 2005 wa kundi "Waandishi wa Habari Wanawake wasiokuwa na vituo."

Ellen Johnson Sirleaf,rais wa Liberia na tuzo ya amani ya Nobel 2011 pamoja na Leymah Gbowee na Tawakkul Karman.
Ellen Johnson Sirleaf,rais wa Liberia na tuzo ya amani ya Nobel 2011 pamoja na Leymah Gbowee na Tawakkul Karman. My Hero
Matangazo ya kibiashara

Tuzo ya Nobel ya Amani 2011 imetolewa kwa Ellen Johnson Sirleaf, Rais wa Liberia, Leymah Gbowee, pia kutoka Liberia, na Yemen Tawakkul Karman kwa harakati zao zisizo na vurugu pamoja na mapambano kwa ajili ya usalama wao na haki za wanawake.

Ellen Johnson Sirleaf ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa rais wa nchi za Afrika. Nae Gbowee Leymah amepewa tuzo hilo kutokana na kazi yake katika kuhamasisha na maandalizi ya wanawake wa makabila yote na dini zote za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika uchaguzi.

Upande wake Tawakkul Karman, kamati ya Nobel imempa tuzo hilo baada ya kuonekana kuwa tofauti kati ya mwanamke ambaye alifanya kazi kwa demokrasia ya amani, na haki za wanawake kabla na wakati wa maandamano katika nchi za Kiarabu.

Kamati ya Nobel imependekeza tuzo hizo tatu zilizotolewa kwa wanawake hao iwe matumaini kwamba zinasaidia kukomesha unyanyasaji wa wanawake katika nchi nyingi na kutoa uwezekano mkubwa kuwa wanawake kwakuwa wanaweza kuwakilisha jamii kwa hali ya amani na demokrasia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.