Pata taarifa kuu
MISRI-MUBARAK

Raisi wa zamani wa Misri Hosni Mubarak athibitika kuwa na Saratani ya tumbo

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani kwa maandamano miezi kadhaa iliyopita amebainikwa kuwa ana saratani ya tumbo, mwanasheria wake Farid al-Dib amedhibitisha.

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak Reuters/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ambaye anatibiwa katika hospitali ya Red Sea mjini Sharm el-Sheikh, alilazwa hospitalini hapo miezi miwili iliyopita baada ya kuanza kuhojiwa na maofisa usalama kuhusiana na tuhuma za rushwa kabla ya kuanza kusumbuliwa na matatizo ya moyo na kukimbizwa hospitali.

Bwana Mubarak amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya hata kabla ya kung'olewa madarakani kwani mnamo mwezi March mwaka huu, rais huyo alielkea nchini Ujerumani kupatiwa matibabu ya kibofu cha mkojo yaliyosababisha kuwa nje ya nchi kwa majuma kadhaa.

Wakili wa bwana Mubarak ameongeza kuwa mteja wake kwasasa hawezi kukabiliana na kesi yoyote kwa kuwa hali yake imeendelea kudhoofu siku hadi siku na kuongeza kuwa mbali na kubainika ana saratani kiongozi huyo pia anakabiliwa na saratani ya ubongo.

Taarifa hizo za kuugua kwa Mubarak zinakuja wakati ambapo serikali ya nchi hiyo imeshafungua kesi ya Rushwa na unyanyasaji dhidi ya bwana Mubarak na watoto wake, kesi inayotarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi wa nane tarehe tatu.

Licha ya taarifa hizo za kuendelea kudhoofu kwa hali ya kiongozi huyo, mwendesha mashtaka wa serikali ameendelea kusisitiza kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kama ilivyopangwa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa huenda kesi hiyo inaweza isifanyike endapo hali ya kiongozi huyo itaendelea kuwa mbaya.

Mwezi wa tano mwaka huu bwana Mubarak alifikisha umri wa miaka 83.

Wakati huohuo baadhi ya wananchi wameendelea kuonekana mjini cairo wakiendelea kushinikiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa viongozi wa zamani waliokuwa chini ya utawala wa Rais Mubarak.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.