Pata taarifa kuu
AFGHANSTANI

Shambulio la Taliban laua watu 36

Takribani watu thelathini na sita wameuwawa na wengine ishirini wamejeruhiwa katika mapigano baina ya wanamgambo wa Taliban na wafanyakazi wa kampuni moja ya ujenzi ,mapigano yaliyodumu kwa saa kadhaa.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea mashariki mwa jimbo la Paktia karibu na mpaka wa Pakistan majira ya saa nane usiku kwa saa za Afghanstani.

Shambulio hilo ni baya zaidi kutokea  baada ya tukio lililotokea mwezi  February mwaka huu ambapo Taliban ilishambulia Benki moja katika eneo la jalalabad na kusababisha vifo vya watu thelathini na wanane wakiwemo maafisa wa polisi waliokuwa wakichukua mishahara yao.

Mkurugenzi wa kampuni ya Galaxy Sky ambayo wafanyakazi wake wameuwawa ameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa hafahamu chanzo cha wafanyakazi wake kushambuliwa.

Taliban imekuwa ikikwamisha mipango mbalimbali ya serikali ya Afghanstani ikiwa ni harakati za kuupunguzia uwezo uongozi wa rais Hamid Karzai na mara kwa mara wamekuwa wakiwateka wafanyakazi wa kigeni.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.