Pata taarifa kuu
PAKISTANI

Taliban yafanya shambulizi la kwanza nchini Pakistani kulipiza kisasi cha kifo cha Osama Bin Laden

Watu 80 wamepoteza maisha nchini Pakistani huku wengine 140 wakijeruhiwa katika mashambalizi mawili ya kulipiza kisasi cha kifo cha Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Duniani Osama Bin Laden yaliyofanywa na Wanamgambo wa Taliban.

Shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa na Wanamgambo wa Taliban nchini Pakistan katika wilaya ya Charsadda
Shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa na Wanamgambo wa Taliban nchini Pakistan katika wilaya ya Charsadda REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Taliban nchini Pakistani Ehsanullah Ehsan amethibitisha huu ni mpango wao kwanza kuteleka katika kulipa kisasi cha kifo cha Osama huku akiahidi mashambulizi zaidi katika nchi za Pakistani na Afghanistani.

Ehsan ametoa kauli hiyo akiwa hajulikani ameweka makazi yake wapi amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya mashambulizi mengi zaidi ili kuonesha ghadhabu waliyonayo kutokana na kuawa kwa Osama.

Watu waliojitoa mhanga kwenye mashambulizi hayo mawili wanaeleza kujilipua katika Mji wa Shabqadar ambao ni moja ambao umekuwa ukishambulia na Mtandao wa Al Qaeda na Taliban kwa mara kadhaa.

Kundi la Wanamgambo wa Taliban nchini Pakistani kwa sasa linaongozwa na Hakimullah Mehsud ambaye alichukua nafasi ya Baitullah Mehsud ambaye aliuawa mwaka 2009 kwenye mashambulizi ya majeshi ya Marekani.

Waziri anayeshughulikia Masuala ya Jimbo la Khyber Paktunkhwa Bashir Ahmed amethibitisho hivyo hivyo 80 na kusema miongoni mwao ni pamoja na raia 11 waliokuwa katika eneo hilo.

Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Charsadda Nisar Khan Marwat ameweka bayana mashambulizi yote mawili yamefanywa na watu waliokuwa kwenye pikipiki.

Nao mashuhuda wa matukio hayo wamesema walisikia sauti ikisema “Mungu Mkubwa” na kisha kufuatiwa na mlipuko mkubwa ambao umesababishwa vifo hivyo vya watu 80.

Tayari Kiongozi wa Juu wa Jeshi nchini Pakistani Jenerali Khalid Shameem Wynne ameahirisha safari yake ya kuelekea nchini Marekani na tayari serikali imetangaza hatua ya kuimarishwa kwa usalama katika nchi hiyo.

Osama Bin Laden aliuawa na Makomandoo wa Marekani tarehe 2 ya mwezi May katika operesheni maalum iliyofanyika nchini Pakistani na kukuta alikuwa anaishi karibu na Kambi ya Jeshi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.