Pata taarifa kuu

China yakataa 'kuunga mkono vikwazo' dhidi ya Korea Kaskazini

China imesema siku ya Ijumaa kuwa inakataa "kuunga mkono vikwazo" dhidi ya Korea Kaskazini, baada ya kujiepusha na kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo Urusi ilipinga kuanzishwa upya kwa kamati ya ufuatiliaji wa vikwazo inayoilenga Pyongyang. 

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akitembelea kiwanda cha kutengeneza silaha huko Korea Kaskazini, Februari 14, 2024.
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un akitembelea kiwanda cha kutengeneza silaha huko Korea Kaskazini, Februari 14, 2024. © KCNA VIA KNS / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hali ya sasa kwenye rasi ya Korea bado ni ya wasiwasi na kuwekewa vikwazo hakuwezi kutatua tatizo," amesema Lin Jian, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China.

Mjumbe wa China alionya siku ya Alhamisi dhidi ya vikwazo vikali zaidi vinavyolenga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK).

Hali ya sasa kwenye Rasi ya Korea ni ya mivutano inayoendelea na makabiliano yanayoongezeka ambayo hayana maslahi ya mtu yeyote. Hili ndilo jambo la mwisho ambalo China inataka, alisema Geng Shuang, naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa.

"Utatuzi wa suala hili hauwezi kutenganishwa na ujenzi wa uaminifu wa kisiasa wa pande zote na hali nzuri. Kuimarisha kwa vikwazo visivyoeleweka na shinikizo haitasaidia kutatua matatizo, lakini badala yake itakuwa kinyume. Kujiingiza katika mantiki ya muungano wa kijeshi na kuhangaishwa na makabiliano kutazidisha tu uhasama na mivutano, na kufanya lengo la kuondoa silaha za nyuklia na kudumisha amani na utulivu katika peninsula kuwa ngumu zaidi " , aliongeza.

"China kwa mara nyingine tena inatoa wito kwa pande zote kuchukua mtazamo wa kimantiki na kivitendo, kubaki na dhamira ya dhati ya suluhu la kisiasa la suala hilo, kuanzisha tena mawasiliano, kuimarisha kuaminiana, kuanzisha upya mazungumzo haraka iwezekanavyo na "kufanya zaidi kwa ajili ya amani na utulivu katika rasi ya Korea. Jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Baraza la Usalama, pia vinapaswa kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya jambo hili," alisema katika ufafanuzi wa kura hiyo, muda mfupi baada ya Baraza la Usalama kupigia kura rasimu ya azimio lililotaka kuongeza muda wa Jopo la Wataalam Kusaidia Tume ya Vikwazo ya DPRK.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.