Pata taarifa kuu

Kiongozi wa upinzani Urusi Navalny yuko katika katika jela la Arctic

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi an mkosoaji mkubwa wa Rais Vladimir Putin, anayezuiliwa Alexeï Navalny, ambaye ndugu na rafiki zake hawajasikia taarifa yoyote kutoka kwake kwa karibu wiki tatu, yuko katika koloni la adhabu huko Kharp, katika Arctic ya Urusi, msemaji wake amesema siku ya Jumatatu.

Alexei Navalny kupitia kiungo cha video kutoka kwa koloni la adhabu la IK-2 huko Pokrov, Mei 17, 2022.
Alexei Navalny kupitia kiungo cha video kutoka kwa koloni la adhabu la IK-2 huko Pokrov, Mei 17, 2022. REUTERS - EVGENIA NOVOZHENINA
Matangazo ya kibiashara

 

"Tulimpata Navalny. Yuko katika chumba nambari 3 katika koloni la adhabu katika eneo la Kharp," amesema msemaji wa kiongozi huyo wa upinzani nchini Urusi, Kira Larmych, Jumatatu kwenye X (zamani ikiitwa Twitter), akibaini kwamba "anaendelea vizuri" na kwamba wakili wake alimtembelea wakati mapema mchana.

Kharp, mji mdogo wenye wakaazi karibu 5,000, unapatikana Yamalo-Nenetsia, eneo la mbali kaskazini mwa Urusi. Ni eneo ambalo liko nje ya Arctic Circle na jela kadhaa za adhabu zinapatikana katika eneo la Kharp.

Alexeï Navalny, mwanaharakati anayepambana na rushwa na mkosoaji mkubwa wa Vladimir Putin, anatumikia kifungo cha miaka 19 jela kwa "itikadi kali". Ndugu na washirika wake hawakuwa na taarifa yoyote kutoka kwake tangu mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, hali ambayo ilimaanisha uhamisho wake kutoka kwa jela la mkoa wa Vladimir, kilomita 250 kutoka Moscow, ambako alikuwa anazuiliwa hadi sasa.

Kwa mujibu wa hukumu ya "itikadi kali" iliyotamkwa dhidi ya Bw. Navalny, mpinzani lazima atumike kifungo chake katika jela "lenye mfumo maalum", jela lenye mfumo ambao masharti ya kizuizini ni magumu zaidi na ambapo kwa kawaida ni wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha jela na wafungwa hatari zaidi wanakozuiliwa. 

"Tangu mwanzo, ilionekana wazi kuwa viongozi walitaka kumtenga Alexei, hasa kabla ya uchaguzi wa urais" uliopangwa kufanyika mwezi Machi 2024, mmoja wa washirika wake wa karibu, Ivan Zhdanov, amejibu kwenye mtandao wa X.

Kukosekana kwa taarifa kutoka kwa kiongozi huyu wa upinzani nchini Urusi kulizusha wasiwasi mkubwa kwa nchi za Magharibi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.