Pata taarifa kuu

Rais wa Korea Kusini, Yoon Suk-yeol, anazuru nchini Saudi Arabia.

Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Korea Kusini kuzuru Riyadh.

Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Korea Kusini kuzuru Riyadh.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa Korea Kusini kuzuru Riyadh. AFP - TATAN SYUFLANA
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo anatarajiwa kujadiliana na mwana mfalme Mohammed Ben Salman, kuhusu ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili, ambao umeonekana kukuwa mwaka huu.

Sawa na jirani yake China, Korea Kusini kwa sasa inaonekana kuanza kuegemea nchi za Ghuba kwa malengo ya masula ya nishati.

Rais Yoon Suk-yeol ameandamana na wawakilishi kutoka makampuni ya nchini Korea Kusini kama vile Samsung, Hyundai na Hanhwa. 

Kando na ziara ya kawaida, safari hiyo imetajwa kuwa ya kibiashara.

Mwaka moja uliopita, mataifa hayo mawili yalitia siani mikataba 26 ya uwekezaji wenye thamani ya bilioni 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.