Pata taarifa kuu

Iran: Ni mwaka mmoja leo tangu kuuawa kwa Mahsa Amini mikononi mwa polisi

Nchini Iran, ni mwaka mmoja leo tangu kuuawa kwa Mahsa Amini, mwanamke mwenye umri wa miaka 22, aliyekamatwa na maafisa wa usalama jijini Tehran, kwa madai ya kutovalia hijabu kwa mujibu wa sheria za serikali. 

Mwanamke huyo baada ya kukamatwa, alipatikana ameuawa, mikononi mwa maafisa wa usalama na kuzua maandamano makubwa jijini Tehran
Mwanamke huyo baada ya kukamatwa, alipatikana ameuawa, mikononi mwa maafisa wa usalama na kuzua maandamano makubwa jijini Tehran REUTERS - ANUSHREE FADNAVIS
Matangazo ya kibiashara

Mwanamke huyo baada ya kukamatwa, alipatikana ameuawa, mikononi mwa maafisa wa usalama na kuzua maandamano makubwa jijini Tehran. 

Baada ya kukamatwa, alipelekwa kwenye kituo maalum, ili kupata utaratibu wa namna ya kuvaa lakini, baadaye alionekana akizirai na kukukimbizwa hospitalini, alikofariki dunia baada ya muda mfupi. 

Polisi walidai kuwa mwanamke huyo alipoteza maisha kwa sababu ya matatizo yake ya  kiafya, sababu ambazo hata hivyo ilikataliwa na wazazi wake na wanaharakati, wakiwatuhumu maafisa wa usalama kwa kusababisha kifo chake. 

Maandamano yalizuka jijini Tehran na baadaye katika mji alikozaliwa wa Saqqez
Maandamano yalizuka jijini Tehran na baadaye katika mji alikozaliwa wa Saqqez © @Reuters

Maandamano yalizuka jijini Tehran na baadaye katika mji alikozaliwa wa Saqqez, kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi na kusababisha makabiliano na maafisa wa usalama. 

Wanaharakati wa haki za kibinadamu kutoka nje za nchi, waliripoti kuwa watu zaidi ya 500 waliuawa wakati wa maandamano hayo, wakiwemo watoto 70, huku maelfu wakikamatwa, kabla ya kupewa msamaha mwezi Februari na  kiongozi wa kiroho, Ali Hosseini Khamenei. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.