Pata taarifa kuu

Jaribio la kwanza la satelite ya kijasusi ya Korea Kaskazini lakosa kufanikiwa.

NAIROBI – Korea Kaskazini imekiri kuwa, jaribio la satelite yake ya kwanza ya kijasusi iliyorushwa angani imeanguka baharini.

Korea Kaskazini imekiri kuwa, jaribio la satelite yake ya kwanza ya kijasusi iliyorushwa angani imeanguka baharini
Korea Kaskazini imekiri kuwa, jaribio la satelite yake ya kwanza ya kijasusi iliyorushwa angani imeanguka baharini AP - Ahn Young-joon
Matangazo ya kibiashara

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Korea Kaskazini imesema ajali ndio iliyosabisha satelite yake kuanguka na sasa inapanga kuirusha tena katika siku zijazo

Hatua hii imekuja baada ya hapo awali, kutangaza kuwa, ilikuwa imepanga kurusha Satelite yake tarehe 11 mwezi Juni, kwa lengo la kuchunguza shughuli za jeshi la Marekani.

Jaribio hili lilikuwa limeanza kuzua hali ya wasiwasi katika mataifa jirani ya Korea Kusini, huku Japan ikitoa tahadhari kwa wakaazi wa mji wa Okinawa.

Jijini Seoul watu walikuwa wamearifiwa wawe tayari kwa zoezi la kuhamishiwa katika maeneo salama, lakini tahadhari hiyo ikaondolewa baada ya dakika 20 kufuatia maelezo ya maafisa kuwa ilitumwa kimakosa.

Marekani, Korea Kusini na Japan zimelaani jaribio hilo la Korea Kaskazini, walilosema linavunja zuia la Baraza la Usalama la Uloja wa Mataifa.

Aidha, Marekani imeitaka Korea Kaskazini kuachana na vitendo vya kichokozi, ikisisitiza kuwa itachukua hatua zote za kujilinda pamoja na washirika wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.