Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini kurusha setilaiti yake ya kijasusi mwezi ujao

NAIROBI – Korea Kaskazini juma hili imesema mwezi ujao itarusha setilaiti yake ya kijasusi katika kile utawala wa Pyongyang umesema ni muhimu kufuatilia mienendo ya hatari ya jeshi la Marekani na washirika wake.

 Kim Jong-un, Rais wa Korea Kaskazini
Kim Jong-un, Rais wa Korea Kaskazini AP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, uongozi wa jeshi la Korea Kaskazini umekosoa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Seoul, ukisema vitendo hivyo ndivyo vimelisukuma taifa hilo kuunda setilaiti hiyo.

Tangazo hili limetolewa siku moja baada ya Japan kuthibitisha kupokea barua ya Pyongyang, ukiutaarifu Tokyo kuwa urushwaji wa chombo hicho utafanyika karibuni, kitendo ambacho Japan imesema kinakiuka vikwazo vya umoja wa Mataifa.

Wataalamu wa masuala ya usalama wanasema ikiwa Korea Kaskazini itafanikiwa kurusha setilaiti yake angani, itakuwa ni hatua kubwa kijeshi kwa taifa hilo, baada ya kufanikiwa kurusha makombora kadhaa ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba nyuklia.

Mwaka 2012 na 2016 Pyongyang ilijaribu kombora lake la masafa marefu ililosema ni Setilaiti, ambapo lilisafiri kupitia kusini mwa nchi ya Japan kwenye mkowa wa Okinawa.

Hatua hii si ya kawaida kuchukuliwa na Pyongyang ambayo aghalabu imekuwa haitoi taarifa ya awali kuhusu mpango wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.