Pata taarifa kuu

Idadi ya watu waliofariki nchini Myanmar baada ya kimbunga Mocha imefikia 60

Nairobi – Takribani watu 60 wamefariki nchini Myanmar baada ya kimbunga kikali..Hii ni baada ya Kimbunga Mocha kutua  Jumapili alasiri katika jimbo la Rakhine la Myanmar karibu na kitongoji cha Sittwe kikiambatana na upepo wa hadi kilomita 209 kwa saa, idara ya hali ya hewa ya Myanmar ilisema.

Kimbunga Mocha kiliikumba Burma mnamo Mei 14, 2023 na kuua takriban watu watatu nchini humo.
Kimbunga Mocha kiliikumba Burma mnamo Mei 14, 2023 na kuua takriban watu watatu nchini humo. AP
Matangazo ya kibiashara

Dhoruba hiyo awali ilipita kwenye kisiwa cha Saint Martins cha Bangladesh, na kusababisha uharibifu na majeruhi, lakini kiligeuka kutoka pwani ya nchi kabla ya kugeuza mwelekeo.

Usiku ulipoingia, ukubwa wa uharibifu huko Sittwe uilikua mkubwa.

Mapema siku hiyo, upepo mkali ulibomoa minara ya mawasiliano ya simu, na kukata mawasiliano katika sehemu kubwa ya eneo hilo. Katika video zilizokusanywa na vyombo vya habari kabla ya mawasiliano kukatika, maji mengi yalipita barabarani huku upepo ukipiga miti na kung'oa mbao kwenye paa za nyumba.

 

Katika nchi jirani ya Bangladesh, maafisa waliiambia AFP kwamba hakuna mtu aliyekufa katika kimbunga hicho, ambacho kilipita karibu na kambi kubwa za wakimbizi ambazo zinahifadhi karibu milioni moja ya  raia wa Rohingya ambao walikimbia ukandamizaji wa jeshi la Myanmar mnamo 2017.

   "Ingawa athari za kimbunga hicho zingeweza kuwa mbaya zaidi, kambi za wakimbizi zimeathirika pakubwa, na kuwaacha maelfu wakihitaji msaada," Umoja wa Mataifa ulisema wakati ukitoa ombi la dharura la usaidizi Jumatatu jioni.

Vimbunga katika Atlantiki ya Kaskazini au vimbunga Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki ni tishio la mara kwa mara na hatari kwenye pwani ya kaskazini mwa Bahari ya Hindi ambapo makumi ya mamilioni ya watu wanaishi.

Shirika lisilo la faida la ClimateAnalytics lilisema kuongezeka kwa halijoto kunaweza kuchangia nguvu ya Kimbunga Mocha.

"Tunaweza kuona halijoto ya bahari katika Ghuba ya Bengal katika mwezi uliopita imekuwa juu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita," Peter Pfleiderer wa kundi hilo alisema.

   "Bahari zenye joto huruhusu dhoruba kukusanya nguvu, haraka, na hii ina matokeo mabaya kwa watu."

   Siku ya Jumanne, mawasiliano yalikuwa yakirejeshwa polepole na Sittwe, ambayo ni makazi ya watu wapatao 150,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.