Pata taarifa kuu

Waandamanaji nchini Pakistan wamtaka jaji mkuu kijiuzulu kufuatia kesi yake Imran Khan

Nairobi – Mamia ya waandamanaji wanaoiunga mkono serikali ya Pakistan wanamtaka jaji mkuu kujiuzulu baada ya kumuachia waziri mkuu wa zamani, Imran Khan, aliyefikishwa mahakamani wili iliyopita.  

Waandamanaji wa Kashmiri wapambana na polisi wa India huko Srinagar Julai 30, 2010.
Waandamanaji wa Kashmiri wapambana na polisi wa India huko Srinagar Julai 30, 2010. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Imran Khan, alikamatwa siku ya Jumanne kufuatia miezi kadhaa ya mgogoro wa kisiasa, na kusababisha wafuasi wake kuandamana katika miji mbalimbali nchini humo.

Hata hivyo,mahakama ilitangaza kuwa kukamatwa kwa kiongozi huyo  ni kinyume cha sheria.

Wiki iliyopita vizuizi na uharibifu  ulishuhudiwa Peshawar kufuatia maandamano kupinga kukamatwa kwake Khan .

Wanasiasa wa Pakistan wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara na kuwekwa rumande tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka 1947, lakini ni wachache walilipinga moja kwa moja jeshi ambalo limefanya angalau mapinduzi matatu na kutawala kwa zaidi ya miongo mitatu.

Kufikia sasa  watu nane waliuwawa na wengine elfu 2000 kukamatwa na polisi baada ya vurugu hizo.Waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif ,amewaamuru polisi nchini humo kuwasaka raia wote waliosababisha vurugu baada ya kukamatwa kwake Imran Khan siku ya jumanne.

Wafuasi wa Khan wanasemakana kusababisha hasara baada ya kulichoma moto jengo la kituo cha televisheni ya taifa na vilevile kuharibu mabasi ya usafiri.

Khan aliachiliwa kwa dhamana baada ya kesi yake kuhusu ufisadi kusikilizwa katika mahakama ya Islamabad.

Mwaka jana pia Imran Khan alikamatwa tarehe 9 Mei .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.