Pata taarifa kuu

Polisi nchini Pakistan kuwasaka wafuasi wa Imran Khan waliosababisha vurugu

Nairobi – Takribani watu nane waliuwawa na wengine elfu 2000 kukamatwa na polisi baada ya vurugu nchini Pakistan.Waziri Mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif ,amewaamuru polisi nchini humo kuwasaka raia wote waliosababisha vurugu baada ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa zamani, Imran Khan siku ya jumanne.

Mahakama ya Juu zaidi ya Pakistan imebatilisha kifungo cha aliyekuwa waziri mkuu Imran Khan. Kwa picha, wafuasi wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, wanaadhimisha uamuzi wa Mahakama ya Juu, huko Peshawar, Pakistan, Alhamisi, Mei 11, 2023.
Mahakama ya Juu zaidi ya Pakistan imebatilisha kifungo cha aliyekuwa waziri mkuu Imran Khan. Kwa picha, wafuasi wa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan, wanaadhimisha uamuzi wa Mahakama ya Juu, huko Peshawar, Pakistan, Alhamisi, Mei 11, 2023. AP - Muhammad Sajjad
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Khan wanasemakana kusababisha hasara baada ya kulichoma moto jengo la kituo cha televisheni ya taifa na vilevile kuharibu mabasi ya usafiri.

Khan aliachiliwa kwa dhamana baada ya kesi yake kuhusu ufisadi kusikilizwa katika mahakama ya Islamabad.Mahakama hiyo ilisema kuwa kukamatwa kwa Khan ni kinyume na sheria.

Mwaka jana pia Imran Khan alikamatwa tarehe 9 Mei baada ya shirika la kupambana na ufisadi la Pakistan, Ofisi ya Kitaifa ya Uwajibikaji, kumshtaki kwa ufisadi.

Polisi wamsindikiza Imran Khan mahakamani baada ya kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi mei 12,2023
Polisi wamsindikiza Imran Khan mahakamani baada ya kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi mei 12,2023 AFP - AAMIR QURESHI

 

Maafisa wa serikali wanadai kuwa Bw Khan na mkewe walipokea ardhi yenye thamani ya mamilioni ya dola kama hongo kutoka kwa tajiri anayemiliki majumba kupitia shirika la uhisani.

Inajulikana kama kesi ya Al-Qadir Trust. Bw Khan na wasaidizi wake wamekana kufanya makosa yoyote.Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 70 anasema mashtaka hayo yanachochewa kisiasa. Anashutumu vyama vya siasa kwa kuunganisha nguvu na jeshi lenye nguvu la nchi hiyo ili kumuondoa mamlakani.

Serikali ya sasa inadai kuwa badala ya kuweka £190m ($240m) kwenye hazina ya Pakistan, serikali ya Imran Khan iliitumia kulipa faini iliyotozwa na mahakama ya Pakistani dhidi ya Bw Hussain kwa kunyakua ardhi ya serikali kinyume cha sheria kwa thamani ya chini ya soko nchini Pakistani katika mji wa Karachi.

Waziri wa mambo ya ndani anadai kuwa Bw Hussain alitoa ardhi ya Jhelum kwa Al-Qadir Trust ili kufanyiwa mapendeleo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.