Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan akamatwa

NAIROBI – Aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan, Imran Khan, amekamatwa wakati akiwasilishwa mahakamani katika jiji la Islamabad, ili kujibu moja ya kesi zinazomkabili tangu kuondolewa mamlakani mwaka 2022.

Aliyekuwa waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu - Islamabad
Aliyekuwa waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu - Islamabad REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI), wamewataka wafuasi wake kuandamana baada yake kukamatwa, lakini polisi wameonya kwamba amri ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu zaidi ya wanne itatekelezwa vikali.

Tulipofika kwenye chumba cha kujitambulisha kielektroniki, kwa kutumia kidole kuashiria mahudhurio, askari kadhaa walitushambulia," amesema Ali Bukhari, wakili wa PTI, akiongeza kuwa walimpiga na kumtoa nje.

Kukamatwa kwake kunakuja baada ya miezi kadhaa ya mzozo wa kisiasa na kunakuja saa chache baada ya jeshi lenye nguvu kumkemea Khan, kutokana na madai kuwa ofisa mmoja mkuu meja jenerali, Faisal Naseer, alihusika katika njama ya kumuua, katika kipindi ambacho alipigwa risasi mguuni mwaka jana.

Karipio hilo la Jumatatu jioni lilisisitiza jinsi uhusiano wa Khan ulivyozorota na jeshi lenye nguvu, ambalo liliunga mkono kuibuka kwake madarakani mnamo 2018 lakini liliondoa uungwaji mkono wake kabla ya kura ya bunge ya kutokuwa na imani iliyomuondoa madarakani mwaka jana.

Taarifa kutoka idara ya mahusiano ya umma ya jeshi, imeyakashfu madai hayo, ikisema ni ya kubuni na yenye nia mbaya.

Huu ulikuwa ni mtindo kwa mwaka jana ambapo maafisa wa kijeshi na mashirika ya kijasusi wanalengwa kwa maneno na propaganda za kustaajabisha kwa ajili ya kuendeleza malengo ya kisiasa, imesema taarifa hiyo.

Serikali ya Pakistani imesema jaribio hilo la kumuua Khan, lilikuwa ni njama ya mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki, ambaye sasa yuko kizuizini na ambaye alikiri katika video iliyovujishwa kwa njia ya kutatanisha kwa vyombo vya habari, lakini mara kwa mara Khan amekataa matokeo ya uchunguzi uliofanyika kuhusu tukio hilo.

Jeshi la Pakistan, ambalo ni la sita kwa ukubwa duniani, lina ushawishi kwa taifa hilo, na limefanya mapinduzi yasiyopungua matatu tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1947 na kutawala kwa zaidi ya miongo mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.