Pata taarifa kuu

India:Ajali ya Boti yasababisha vifo vya watu 22 na majeruhi 6

Nairobi – Watu 22 wamefariki baada ya boti ya utalii  waliokua wakisafiria kuanguka nchini India.Kulingana na taarifa ni kuwa wengi wa waliokuwa ndani ya boti hilo ni watoto waliokuwa katika matembezi baada ya kufunga shule. .

Miili ya wahamiaji haramu wapatao 94 kutoka Barani Afrika waliopoteza maisha baada ya kuzama kwa boti waliyokuwa wanasafiria
Miili ya wahamiaji haramu wapatao 94 kutoka Barani Afrika waliopoteza maisha baada ya kuzama kwa boti waliyokuwa wanasafiria REUTERS/Gang Jae-Nam/Newsis
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa hakuna taarifa kamili ya chanzo cha ajali hiyo iliyotokea katika jimbo la kusini la wilaya ya Malappuram huko Kerala kusini mwa India.

Shughuli ya uokoaji bado inaendelea wakati huu watu sita wakiwa hospitalini. Kulingana na wanaoedesha shughuli hiyo ni kuwa wameopoa miili 22 wakiwemo wanawake 15 na wanaume saba.Kati ya miili hiyo 22 kumi na moja ni kutoka kwa familia moja.

Rajisa, ambaye alikuwa kwenye boti hiyo pamoja na mumewe na bintiye, alisema kuwa  abiria wengi waliokuwa ndani ya boti hiyo walikuwa watoto na kwamba alishuhudia moshi ukitoka kwenye boti hili wakati wa safari.

"Tulinusurika kwa sababu tu tulikuwa tumevaa jaketi la kujiokoa," Rajisa, ambaye alijeruhiwa shingo baada ya kugonga boti, alinukuliwa akisema.

Alisema jaketi tatu za kujiokoa zililetwa kwake na familia yake. "Boti iliyumba wakati fulani baada ya kuanza safari. Kila mtu alitupwa upande mmoja huku mashua ikiyumbayumba," aliiambia Onmanorama.

"Nilianguka mbele ya mtoto wangu na kuzama majini. Boti ilipinduka juu ya watu waliokuwa wameanguka majini. Kulikuwa na watoto wengi kwenye boti," alisema.

Taarifa zinasema kuwa  wafanyikazi kutoka Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Maafa na Walinzi wa Pwani ya India, walikuwa wakitumia kamera za chini ya maji kuwatafuta wale ambao bado hawajulikani walipo.

VD Satheesan, mwanasiasa kutoka chama cha upinzani cha Congress katika jimbo hilo, alisema ajali hiyo "ilisababishwa na mwanadamu" na akataka uchunguzi ufanyike.

"Hakuna hata anayejua kama boti hiyo ilikuwa na leseni au la," alisema alipokua , akizungumza na waandishi wa habari.Kesi imesajiliwa dhidi ya mmiliki wa boti hiyo kwa madai ya mauaji ya bila kukusudia, ripoti za vyombo vya habari zilisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.