Pata taarifa kuu

Rais Erdogan arejea kwenye kampeni za uchaguzi baada ya kuugua

NAIROBI – Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki, siku ya Jumamosi ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza ndani ya siku tatu, baada ya matatizo ya tumbo kumfanya asiendeleze kampeni, katika kipindi hiki muhimu kuelekea uchaguzi wa Mei 14.

Rais Recep Erdogan akiwa kwenye kampeni Instabul, Uturuki, Aprili 29, 2023
Rais Recep Erdogan akiwa kwenye kampeni Instabul, Uturuki, Aprili 29, 2023 © @RTErdogan
Matangazo ya kibiashara

Erdogan mwenye umri wa miaka 69, katika kampeni zake hivi leo kwenye tamasha la Instabul, ameandamana na wandani wake wa karibu, akiwemo rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev na waziri mkuu wa Libya, Abdelhamid Dbeibah.

Mataifa haya mawili yamekuwa yakipigana vita kwa kutumia ndege zisizo na rubani za Uturuki, ambazo zitakuwa maarufu katika hafla ya anga ya wikendi hii.

Rais Erdogan hajaonekana hadharani tangu kuugua akiwa moja kwa moja kwenye Televisheni usiku wa Jumanne juma hili.

Akihutubu kwenye jukwaa hilo la tamasha la Instabul Jumamosi, Erdogan hajazungumzia masuala ya afya yake, lakini ameelezea juhudi za serikali kusaidia waathiriwa wa tetemeko kubwa la ardhi la Februari lililogharimu maisha ya zaidi ya 50,000.

Kadhalika amesema lengo lake ni kile ameita kuanzisha karne mpya ya Uturuki.

Akabiliwa na upinzani mkubwa

Kura nyingi za maoni zinaonyesha kuwa Erdogan, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Kemal Kilicdaroglu.

Kilicdaroglu ameunda aina ya muungano mpana ambao Erdogan alikuwa amebobea kuunda kwa zaidi ya miaka 20, muungano huu wa upinzani ukijumuisha baadhi ya washirika wa zamani wa Erdogan, waislamu na wazalendo, pamoja na Wakurdi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.