Pata taarifa kuu

Kisa cha moto katika hospitali moja mjini Beijing chaua watu wengi, uchunguzi unaendelea

Uchunguzi unaendelea Jumatano, Aprili 19, siku moja baada ya moto kuzuka katika hospitali moja mjini Beijing na kusababisha vifo vya takriban watu 29 na kuwalazimisha wagonjwa kutoroka kupitia madirisha, vyombo vya habari vya China vimeripoti. Kufuatia tukio hilo watu kumi na wawili wamekamatwa akiwemo mkurugenzi wa hospitali hiyo.

Afisa wa uchunguzi katika eneo la tukio la moto kwenye jengo la hospitali ya Changfeng.
Afisa wa uchunguzi katika eneo la tukio la moto kwenye jengo la hospitali ya Changfeng. AFP - GREG BAKER
Matangazo ya kibiashara

Watu 12 wamekamatwa mjini Beijing siku moja baada ya moto kuzuka katika hospitali moja, tulio lililosababisha vifo vya takriban watu 29, polisi imesema Jumatano (tarehe 19 Aprili). Mkurugenzi wa hospitali na wafanyakazi wa kampuni inayosimamia kazi za ukarabati katika hpspitali hiyo ni miongoni mwa waliokamatwa, amesema Sun Haitao, wa usalama wa umma wa Beijing, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Kulingana na uchunguzi wa awali ulionukuliwa na televisheni ya serikali CCTV, moto huo ulianzishwa na "cheche  wakati wa kazi ya ukarabati wa ndani". Cheche hizi "ziliwasha vitu vyenye kulipuka vya rangi kwenye eneo hili", kulingana na uchunguzi huu. Moto huo uliwalazimu wagonjwa kutoroka kupitia madirishani kwa kutumia shuka na kukimbilia kwa kwa kupitia kwenye viyoyozi kwenye kuta, kulingana na picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kukaguliwa haraka.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.