Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Kazakhstan: Uchaguzi wa mapema wa bunge unaleta matumaini mengi

Uchaguzi wa mapema wa wabunge unafanyika leo Jumapili, Machi 19 nchini Kazakhstan. Takriban wapiga kura milioni 12 wameitwa kupiga kura kuchagua wabunge wa Baraza la Wawakilishi, Majilis, wabuge wamajimbo, Mazlikhats.

Mut kwenye farasi akipita mbele ya ubao wenye mabango rasmi ya kampeni ya wagombea katika ucaguzi wa wabunge Baraza la Wawakilishi na wabunge wa majimbo kwenye barabara ya Almaty, Kazakhstan, Machi 15, 2023.
Mut kwenye farasi akipita mbele ya ubao wenye mabango rasmi ya kampeni ya wagombea katika ucaguzi wa wabunge Baraza la Wawakilishi na wabunge wa majimbo kwenye barabara ya Almaty, Kazakhstan, Machi 15, 2023. REUTERS - PAVEL MIKHEYEV
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Kitaifa lilivunjwa miezi mitatu iliyopita na Rais Tokayev aliyechaguliwa tena mwezi Novemba kwa zaidi ya 80% ya kura katika uchaguzi wa urais bila ushindani. Uchaguzi huo unaibua matumaini mengi miongoni mwa raia wa Kazakhstan, ambao wanatarajia kuona ahadi za mabadiliko ya kidemokrasia na uboreshaji wa nchi hiyo zikiimarishwa.

Kwa bahati mbaya, ilikuwa Machi 19, 2019 ambapo Rais wa zamani Noursultan Nazarbayev, akisimamia Kazakhstan kwa karibu miongo mitatu, aliamua kuachia ngazi. Baada ya maandamano kukandamizwa mwaka jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 230, mrithi wake Kassym Jomart Tokaïev, mshindi wa chaguzi mbili za urais, alizindua mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi.

Mchakato huo ulianza mwezi Juni, kwa kura ya maoni ya kikatiba, iliyopitishwa kwa zaidi ya 75% ya kura, zinazopaswa kufunga enzi ya Nazarbayev na kutoa mamlaka zaidi kwa Bunge.

Chaguzi hizi za wabunge hupangwa kwa mujibu wa kanuni mpya zinazolenga kuhimiza ushindani, hasa utaratibu uliorahisishwa wa usajili wa vyama vya siasa, kiwango cha ustahiki ambacho kinaanzia asilimia 7 hadi 5, uwezekano wa kila mkoa kuwa na mjumbe wa Bunge hilo au hata idhini ya wagombea binafsi kugombea uchaguzi, wa kwanza kwa nchi hii ya Asia ya Kati, mara nne ya ukubwa wa Ufaransa.

Wakosoaji wa utawala huo, hata hivyo, wanakataa kuamini katika nia ya kweli ya kupunguza mamlaka ya rais na kuhimiza vyama vingi. Mwishoni mwa uchaguzi, hata hivyo, vyama viwili vipya, cha ikolojia na mrengo wa kulia, vinapaswa kuingia Bungeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.