Pata taarifa kuu

Bashar al-Assad kukutana kwa mazungumzo na Vladimir Putin Moscow

Bashar al-Assad aliwasili Moscow Jumanne jioni kukutana na mwenzake wa Urusi siku ya Jumatano kuhusu ushirikiano kati ya nchi zao.

Rais wa Syria Bashar al-Assad na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Damascus mwaka 2020.
Rais wa Syria Bashar al-Assad na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Damascus mwaka 2020. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Vladimir Putin anakutana na Bashar al-Assad mjini Moscow Jumatano Machi 15, kulingana na taarifa kutoka Kremlin. Wakuu wa nchi za Urusi na Syria watajadili "maswala muhimu kuhusu maendeleo ya ushirikiano wa Urusi na Syria katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kibinadamu, na pia matarajio ya utatuzi ulioratibiwa wa hali nchini Syria na kote nchini, ” taarifa hiyo imebaini.

Bashar al-Assad aliwasili Moscow Jumanne jioni "kwa ziara rasmi ambapo atakutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin", kulingana na taarifa kutoka ikulu ya rais wa Syria. Bashar al-Assad, "akiambatana na ujumbe mkubwa wa mawaziri", alipokelewa na Mikhail Bogdanov, mwakilishi maalum wa Rais Putin na naibu waziri wa mambo ya nje, ofisi ya rais imeongeza.

Kuelekea 'hali ya kawaida kati ya Damascus na Ankara'

Ziara ya mwisho ya hadhara ya Rais wa Syria mjini Moscow ilifanyika mwezi Septemba 2021, alipozungumza na Bw. Putin. Gazeti linalounga mkono serikali la Al-Watan, likinukuu gazeti la Urusi la Vedomosti, lilisema Jumanne kwamba marais hao wawili wanapaswa kujadili hasa kuhusu "kurejeshwa kwa uhusiano kati ya Damascus na Ankara", ambapo Urusi ina jukumu la mpatanishi.

Mkutano wa pande tatu ulifanyika mwezi Disemba mjini Moscow kati ya mawaziri wa ulinzi wa Uturuki, Syria na Urusi, wa kwanza tangu mwaka 2011. Uhusiano umevunjika tangu kuanza kwa vita nchini Syria mwaka 2011, wakati Uturuki iliunga mkono upande wa makundi ya waasi yanayopinga Damascus. Urusi, mshirika mkuu wa Damascus, kwa upande wake imetoa msaada wa kijeshi kwa jeshi la Syria katika mzozo huo.

Gazeti hilo, likinukuu chanzo hicho hicho, linaamini kwamba "maendeleo ya sasa kuhusu uhusiano wa Syria na nchi za kiarabu" yanapaswa kushughulikiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.