Pata taarifa kuu

Matajiri wawili maarufu nchini Urusi wapatikana wamefariki India

Matajiri wawili wa Urusi wamefariki dunia katika mazingira ya kushangaza nchini India. Milionea Pavel Antov, mkosoaji wa vita vya Ukraine, alipatikana amekufa baada ya kuanguka kutoka dirisha la hoteli moja nchini India mnamo Desemba 24, siku mbili baada ya rafiki yake, Vladimir Budanov, kufa wakati wa safari hiyo. Vyombo vya habari vinashangaa juu ya vifo hivi, ambavyo vinakumbusha vifo kama hivyo vilivyowakuta wapinzani wengine wa Urusi duniani.

Bendera ya Urusi ikipepea juu ya jengo la Bunge huko Moscow.
Bendera ya Urusi ikipepea juu ya jengo la Bunge huko Moscow. AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Pavel Antov alikuwa amekuja kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 66 katika eneo la Rayaga, katika jimbo la Orissa, na bila kueleweka alijitupa kwenye dirisha la hoteli moja kutoka ghorofa ya tatu ya hoteli hiyo. "Alikuwa na huzuni kufuatia kifo cha rafiki yake," amesema mmoja wa marafiki zake wa Kihindi. Polisi wa eneo hilo wanasema huenda tajiri huyo alijiua.

Vyombo vya habari, hata hivyo, vinashuku kwamba huenda Pavel Antov aliuawa kwani kifo chake kinafanana na matajiri wengine wengi wa Urusi ambao walithubutu kusema dhidi ya Vladimir Putin. Pavel Antov alijipatia utajiri wa soseji na inasemekana ana zaidi ya dola milioni 150. Alikuwa mwanachama wa United Russia, chama cha Vladimir Putin. Katika ujumbe wake, hata hivyo, alikosoa vita vya Ukraine. Kisha akaifuta meseji hiyo na kuomba msamaha kabisa.

Diplomasia ya India bado iko kimya kwa sasa

Mwenzake Vladimir Budanov hakujulikana kuwa mkosoaji wa mamlaka ya Urusi. Hata hivyo, pia alikufa, siku mbili mapema, kwa mshtuko wa moyo katika chumba chake. Kifo cha asili, kulingana na madaktari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.