Pata taarifa kuu

Japan yataka kuongeza maradufu matumizi yake ya kijeshi

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida anataka kuimarisha uwezo wa ulinzi wa Japan. Na, kwa mara ya kwanza, anaiomba serikali yake kuandaa bajeti ya ulinzi inayolenga kuongeza matumizi ya kijeshi kutoka 1% hadi 2% ya Pato la Taifa kwa miaka mitano ifikapo 2027. Inabakia kuonekana jinsi anatarajia kufadhili bajeti hii kutokana na udhaifu wa uchumi wa Japan, nchi yenye deni kubwa kuliko nchi zote za kundi la nchi zilizostawi kiuchumi, G7.

Japan inatafuta kuimarisha mkakati wake wa ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka ambavyo inaamini kuwa ni kutoka China na Korea Kaskazini, pamoja na athari za kimataifa za kijiografia za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Japan inatafuta kuimarisha mkakati wake wa ulinzi na usalama ili kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka ambavyo inaamini kuwa ni kutoka China na Korea Kaskazini, pamoja na athari za kimataifa za kijiografia za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. AP
Matangazo ya kibiashara

Matumizi ya kijeshi ya Japan yamekuwa yakipanda kwa miaka kumi, lakini hadi sasa yamekwama hadi 1% ya Pato la Taifa. Kwa mwaka wa kifedha wa 2023-2024, wanapaswa kuwakilisha rekodi mpya, sawa na euro bilioni 39.

Japan inahoji kuhusu lengo la 2% la Pato la Taifa kwa usalama wake tangu miaka kadhaa. Kuongezeka kwa matumizi ya kijeshi huenda ni kinyume na Katiba ya pacifist na wito wa ulinzi wa majeshi ya Japan. Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine unamuwezesha Waziri Mkuu Fumio Kishida kuhalalisha kuongeza maradufu bajeti ya ulinzi katika kipindi cha miaka mitano.

Tangu Urusi ilipovamia Ukraine, Wajapani wengi wanasema wanaunga mkono ongezeko hilo. Wanaona vitisho kutoka nchi kama vile China, Korea Kaskazini na Urusi. Wanahofia kwamba vita vya uvamizi vya Ukraine vitachochea China kuivamia Taiwan. Wanapendelea kupata uwezo wa "counter-attack" kwa silaha zenye uwezo wa kuharibu maeneo ya kurushia makombora ya Korea Kaskazini.

Deni kubwa

Inabakia kuonekana ikiwa Japan ina njia ya kuongeza bajeti yake ya ulinzi maradufu. Deni la nchi ni kubwa, zaidi ya mara mbili na nusu ya ukubwa wa uchumi wake. Gharama zinazohusiana na kuzeeka kwa raia na janga la Uviko-19 ni kubwa. Na udhaifu wa hivi karibuni wa pesa ya China (yen) hausaidii chochote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.