Pata taarifa kuu

Tuzo ya Sakharov ya Bunge la Ulaya yatolewa kwa raia 'jasiri' wa Ukraine

Bunge la Ulaya limetangaza Jumatano kwamba limetoa Tuzo ya Sakharov ya Haki za binadamu ya 2022 kwa raia wa Ukraine, kama ishara ya kuunga mkono uvamizi wa nchi yao na Urusi tangu Februari 24. Mwaka jana, Bunge la Ulaya lilikabidhi tuzo hii kwa mpinzani wa Urusi Alexei Navalny.

Ndege isiyo na rubani imebeba bendera kubwa ya kitaifa mbele ya Mnara wa Kumbusho wa uzalendo huko Kyiv, Ukraine, Jumatano, Agosti 24, 2022.
Ndege isiyo na rubani imebeba bendera kubwa ya kitaifa mbele ya Mnara wa Kumbusho wa uzalendo huko Kyiv, Ukraine, Jumatano, Agosti 24, 2022. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza kuanzishwa kwa sheria ya kijeshi katika maeneo manne yaliyounganishwa. Utawala wa uvamizi wa Urusi huko Kherson, kusini mwa Ukraine, umesema Jumatano kwamba ulikuwa ukiuhamisha wakazi wa mji huo unaokabiliwa na mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine ambao wanaosonga mbele, huku wakihakikisha kwamba jeshi la Urusi litapigana katika mji huo "hadi kifo". Kwa upande wake, Kyiv imeshutumu Urusi kwa "kujaribu kuwatisha" wakazi wa mji wa Kherson.

Naye Kamanda wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine anasema hali katika mji wa kusini wa Kherson ni "ngumu" na wakaazi wanapaswa kuhamishwa.

Jenerali Sergei Surovikin alisema wanajeshi wa Ukraine wanaotumia roketi za Himars walikuwa wakigonga miundombinu na makazi ya jiji hilo. Alizungumza kwenye TV ya serikali ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.