Pata taarifa kuu

India yachunguza tahadhari kuhusiana na dawa nne za kikohozi

Wizara ya Afya nchini India inachunguza tahadhari ya kimataifa imetolewa kuhusu dawa nne za kikohozi baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuonya kuwa zinahusishwa na vifo vya watoto 66 nchini Gambia. 

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi huko Gandhinagar mnamo Julai 29, 2022.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi huko Gandhinagar mnamo Julai 29, 2022. AP - Ajit Solanki
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa watoto wanaotumia dawa hizo, wanapata majeraha ya figo na kusababisha maafa. 

Shirika la afya duniani, WHO, juma hili limetoa angalizo kuhusu matumizi ya dawa nne za kimiminika zinazotumiwa kutibu kikohozi na mafua, ambazo zinatengenezwa na kampuni kutoka nchini India, sharika hilo likisema zinahusishwa na vifo vya watoto 66 nchini Gambia.

WHO kwenye taarifa yake, imeongeza kuwa huenda dawa hizo ambazo zinatatizo, zikawa zimesambazwa nchi ya mataifa ya Afrika Magharibi, huku huenda ikawa imefika kwenye mataifa mengi ulimwenguni.

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, dawa hizo nne ambazo zinaendelea kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara, zinaweza kuwa zilisababisha madhara kwa ini na vifo vya watoto 66.

Tedros, aliongeza kuwa “WHO inafanya kazi kwa karibu na kampuni zinazotengeneza dawa hizo pamoja na mamlaka za India”.

Dawa hizo zilizotajwa ni Promethazine Oral Solution, Kofexmalin Baby Cough Syrup, Makoff Baby Cough Syrup na Magrip N Cold Syrup. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.