Pata taarifa kuu

Ukraine yashutumu jeshi la Urusi kwa kufanya mashambulizi katika eneo la kinu cha nyuklia

Shirika la nyuklia la Ukraine, Energoatom, limeishutumu Urusi kwa kufanya mashambulizi ya anga kwenye eneo la kituo cha nyukliae cha Pivdennonooukrainsk, kusini mwa nchi hiyo, na kuzua hofu kwa mara nyingine tena kuhusu hatari ya kutokea ajali ya nyuklia.

Picha iliyopigwa kutoka kwa CCTV katika kinu cha nyuklia cha Pivdennonoaukrainsk, Septemba 19, 2022.
Picha iliyopigwa kutoka kwa CCTV katika kinu cha nyuklia cha Pivdennonoaukrainsk, Septemba 19, 2022. via REUTERS - ENERGOATOM STATE COMPANY
Matangazo ya kibiashara

"Mnamo Septemba 19, 2022, saa sita na dakika 20 usiku kwa saa za Ukraine, jeshi la Urusi lilifanya mashambulizi ya anga kwenye eneo la viwanda la kinu cha nyuklia cha Pivdennonooukrainsk," shirika la nyuklia la Ukraine, Energoatom, limeandika kwenye Telegram siku ya Jumatatu. "Mlipuko mkubwa ulitokea mita 300 tu kutoka kwa vinu," Energoatom limesema. "Kwa sasa, mitambo mitatu ya kituo cha nyuklia cha Pivdennonooukrainsk inafanya kazi katika hali ya kawaida", Energoatom imebainisha, huku shirika hilo likiongeza kwamba mashambulizi hayo hayakusababisha vifo au hasara yoyote.

Mashambulizi hayo yaliharibu takriban madirisha 100 katika jengo la kituo cha nyuklia na kusababisha kukatika kwa njia tatu za umeme wa juu katika kituo hicho, kulingana na chanzo kimoja.

"Urusi inahatarisha ulimwengu wote"

"Urusi inahatarisha ulimwengu wote. Ni lazima tukomeshe mashambulizi haya kabla hatujachelewa,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwenye Telegram.

Kituo kingine cha nyuklia cha Ukraine, kile cha Zaporizhia, ambacho ni kikubwa zaidi barani Ulaya na kinachokaliwa kwa mabavu na wanajeshi wa Urusi, tayari kilikuwa kikilengwa na mashambulizi ya anga katika miezi ya hivi karibuni, na kusababisha wasiwasi mkubwa katika nchi za Magharibi. Kyiv na Moscow zililaumiana kwa mashambulizi hayo na kulaumiana kwa kuhatarisha hatari ya kutokea kwa ajali ya nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.