Pata taarifa kuu

Tajikistan na Kyrgyzstan zasitisha vita baada ya mapigano makali

Mapigano makali yalizuka kwenye mpaka kati ya Kyrgyzstan na Tajikistan. Watu zaidi ya thelathini walijeruhiwa katika mapigano hayo. Jamhuri hizi mbili za zamani za Soviet wanashtumiana kila upande moja kuhusika katika mapigano ya kila mmoja.

Raia wa Kyrgyzstan waliojitolea wakiwa nje ya jengo la serikali kudai wapelekwe kwenye eneo lenye migogoro huko Bishkek, Kyrgyzstan, Ijumaa, Septemba 16, 2022.
Raia wa Kyrgyzstan waliojitolea wakiwa nje ya jengo la serikali kudai wapelekwe kwenye eneo lenye migogoro huko Bishkek, Kyrgyzstan, Ijumaa, Septemba 16, 2022. AP - Vladimir Voronin
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku kadhaa, mapigano yameongezeka na kuripotiwa kutokea kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili. Mapigano hayo yanaripotiwa kusababisha zaidi ya watu 30 kujeruhiwa na karibu dazeni kuuawa kwa jumla, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Kyrgyzstan imeshutumu Tajikistan kwa "kushambulia kwa ndege za kivita eneo la Kyrgyz" na kuendelea kupeleka "vifaa muhimu", ikiwa ni pamoja na "silaha nzito". Kyrgyzstan imeongeza kujibu "mashambulizi yote ya ardhini na angani". Tajikistan, kwa upande wake, imeshutumu vikosi vya Kyrgyzstan kwa kufyatua risasi mapema Ijumaa kwenye vivuko vya mpaka vya Tajik, bila kuripoti mara moja majeruhi katika safu zake.

Wakazi wa vijiji kadhaa vya mpaka wamekimbia eneo la mapigano, imesema Wizara ya Hali ya Dharura ya Kyrgyzstan, ikitangaza kufunguliwa kwa vituo vya mapokezi. Tawi la shirika la msalaba Mwekundu limesema takriban watu 19,000 wanaoishi karibu na mji wa Kyrgyzstan wa Batken wamehamishwa kwa tahadhari.

Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov na Rais wa Tajik Emomali Rakhmon, ambao walikutana kando ya mkutano wa kilele wa kikanda wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) huko Uzbekistan, wameamuru wanajeshi wao "kuondoka". Usitishaji wa mapigano ulikuja saa nne asubuhi kwa saa za nchi hiyo.

Asubuhi, Urusi ilikuwa imetoa wito kwa mataifa hayo mawili kuchukua "hatua za haraka" kumaliza hali hiyo. Lakini Ijumaa hii jioni, Bishkek na Dushanbe walishutumiana kila mmoja kukiuka makubaliano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.