Pata taarifa kuu

Urusi: Ravil Maganov, kiongozi wa kampuni ya Loukoil, afariki katika mazingira tatanishi

Ravil Maganov ni hivi punde kati ya watendaji wakuu wa makampuni ya Urusi kufariki katika mazingira ya kushangaza. Ravil Maganov, alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya kibinafsi ya mafuta ya Loukoil nchini Urusi.

Kiongozi wa kampuni ya kibinafsi ya mafuta nchini Urusi Ravil Maganov (kulia), akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin, mnamo Novemba 21, 2019 huko Moscow.
Kiongozi wa kampuni ya kibinafsi ya mafuta nchini Urusi Ravil Maganov (kulia), akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin, mnamo Novemba 21, 2019 huko Moscow. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari kadhaa vya Urusi, lakini pia mashirika ya habari ya Interfax na Tass, katika habari zao za kwanza, zilibaini kama sababu ya kifo cha Ravil Maganov "kuanguka kutoka ghorofa ya 6" kupitia dirisha la Hospitali Kuu ya Kliniki huko Moscow. Shirika la habari la Tass baadaye lilifafanua kwamba alijiua. Baadaye kidogo, asubuhi, kampuni hiyo iliandika katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Ravil Maganov alikufa "kutokana na ugonjwa mbaya". Alikuwa na umri wa miaka 67.

Kiongozi wa kihistoria wa kampuni iliyoanzishwa mnamo mwezi wa Novemba 1991, ni yeye ambaye, kulingana na Loukoïl, alifikiria na kupendekeza jina la kampuni hiyo. Mnamo mwezi wa Desemba 2019, alipokea tuzo ya mafanikio ya maisha kutoka kwa rais wa Urusi. Baada ya kutunukiwa tuzo Ravil Maganov alipiga picha pamoja na Vladimir Putin.

Mwezi Machi mwaka huu, kampuni ya mafuta ya Lukoil ilikuwa mojawapo ya makampuni machache ya Kirusi yaliyotaka kukomeshwa kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine. Mwezi mmoja baadaye, mwenyekiti wa kundi hilo, bilionea Vaguit Alekperov, alijiuzulu baada ya kuwekwa kwenye orodha ya watu wa Urusi waliochukuliwa vikwazo na Uingereza.

Watendaji kadhaa wa nishati wa Urusi wamekufa katika hali isiyo ya kawaida katika miezi ya hivi karibuni. Mnamo mwezi wa Aprili, mwili wa makamu wa kiongozi wa zamani wa kampuni ya gesi ya Novatek, Sergey Protosenya, ulipatikana pamoja na ule wa mkewe na binti yao, katika jumba la kifahari la Uhispania. Mwezi huo huo, naibu mwenyekiti wa zamani wa Gazprombank alipatikana amekufa nyumbani kwake huko Moscow; mabaki ya mke wake na binti yao pia yalipatikana kwenye ghorofa. Na mwezi wa Mei, Alexander Subbotin, kiongozi wa zamani wa kampuni ya mafuta Loukoil, alikufa kwa kushindwa kwa moyo, inaonekana baada ya kutafuta matibabu mbadala kutoka kwa waganga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.