Pata taarifa kuu

Antonio Guterres atoa wito wa kurejeshwa kwa nafaka na mbolea za Urusi kwenye masoko

Mbolea na bidhaa za kilimo za Urusi lazima ziwe na uwezo wa kufikia masoko ya dunia "bila kuzuiliwa", katika hatari ya mgogoro wa chakula duniani kuanzia 2023, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Istanbul, siku ya Jumamosi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa Kituo cha Uratibu wa Pamoja (JCC) unaosimamia mpango wa nafaka wa Ukraine huko Istanbul, Agosti 20, 2022.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa Kituo cha Uratibu wa Pamoja (JCC) unaosimamia mpango wa nafaka wa Ukraine huko Istanbul, Agosti 20, 2022. © Khalil Hamra/AP
Matangazo ya kibiashara

"Ni muhimu kwamba serikali na sekta binafsi zishirikiane ili kuzipeleka sokoni," amesema Antonio Guteress kutoka Kituo cha Uratibu wa Pamoja (JCC), ambacho kinasimamia utekelezaji wa makubaliano ya mauzo ya nafaka kutoka Ukraine yaliyotiliwa saini mwezi Julai na Kyiv na Moscow chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa na Uturuki. Mkataba huu pia unahakikisha kwamba Urusi inaweza kuuza nje bidhaa zake za kilimo na mbolea licha ya vikwazo vya nchi za Magharibi.

"Tunachokiona hapa Istanbul na Odessa (usafirishaji wa nafaka za Ukraine ni sehemu inayoonekana zaidi ya suluhisho. Sehemu nyingine ya makubaliano haya ya kina ni upatikanaji usiozuiliwa wa masoko ya dunia ya chakula na mbolea ya Urusi, ambayo hayako chini ya vikwazo," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, akisisitiza kuwa pamoja na kwamba mauzo ya nje ya mbolea ya Urusi na mazao ya kilimo bado yamekutana na "vikwazo" .

"Bila ya mbolea mwaka 2022, kunaweza kusiwe na chakula cha kutosha mwaka wa 2023. Kupata chakula na mbolea zaidi kutoka Ukraine na Urusi ni muhimu katika kutuliza masoko [...] na kupunguza bei kwa watumiaji," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.