Pata taarifa kuu

Marekani yatangaza mazungumzo ya kibiashara na Taiwan, Beijing yapandwa na hasira

Katika mvutano kamili kati ya China na Marekani kuhusu hatima ya Taiwan, Washington ilitangaza Jumatano Agosti 17 kwamba mazungumzo rasmi na Taipei yataanza mwishoni mwa msimu wa joto ili kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara na kiuchumi. Beijing haikuchelewa kulaani tangazo hili na kutishia kujibu. Hata kama biashara yao ni muhimu, hakuna makubaliano ya kibiashara yaliyofikiwa kati ya Taipei na Washington.

Maafisa wa Marekani na Taiwan wakutana kwa mkutano mjini Taipei, wakati wa ziara ya wajumbe wa Marekani mnamo Agosti 15, 2022.
Maafisa wa Marekani na Taiwan wakutana kwa mkutano mjini Taipei, wakati wa ziara ya wajumbe wa Marekani mnamo Agosti 15, 2022. © Ministère taïwanais des Affaires étrangères / via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa, masharti yaliyochaguliwa hayaeleweki na ni ya jumla kwa mazungumzo haya ambayo yataanza msimu huu, kulingana na ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani. Bado hatuzungumzii kuhusu makubaliano ya biashara huria ambayo baadhi ya watu huko Taipei wanaitisha.

Taiwan haijajumuishwa katika Ushirikiano mpya wa Kiuchumi wa eneo la Indo-Pasifiki uliozinduliwa mwezi Mei na Joe Biden. Hii ni kukataa kutowaweka wanachama wengine kumi na tatu katika mvutano na Beijing.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya Mpango wa Biashara wa Karne ya 21 wa Marekani na Taiwan, uliozinduliwa mwezi Juni na Katherine Kai na Waziri wa Taiwan John Deng wakati wa mkutano wa mtandaoni. Tayari Beijing imepandwa na hasira kufuatia tangazo hili la Marekani.

Majibu kwa 'sera na mbinu zisizofaa soko'

Biashara baina ya nchi hizi mbili imekua kwa kasi na kisiwa hicho tangu mwaka 1994 na kutiwa saini kwa mfumo wa biashara na uwekezaji. Mnamo 2020, walifikia kilele cha dola bilioni 106, jambo ambalo linaifanya Taiwan kuwa mshirika wa tisa mkubwa wa kibiashara wa Marekani, hasa kutokana na Taiwan, kupitia tasnia yake ya kiteknolojia, kufanya mauzo ya nje.

Katika hati ya mazungumzo yaliyochapishwa Jumatano, Washington inapendekeza kuimarisha zaidi mawasiliano yake na kutafakari kwa pamoja juu ya majibu ya "sera na mbinu zisizofaa na soko", ambayo wachambuzi wameelewa kama marejeleo ya mazoea ya China.

Beijing 'inapinga vikali'

Beijing ni wazi inachukulia mtazamo hafifu sana wa "mpango huu mpya", ambayo inauona kama ishara ya kuongezeka kwa ushirikiano wa Washington na serikali ya Taiwan, baada ya uungwaji mkono wa kisiasa na ziara ya Nancy Pelosi mwanzoni mwa mwezi huu, anaripoti mwandishi wetu huko Beijing, Stéphane Lagarde.

Kufuatia mzozo huo mpya, uliochochewa na safari ya Rais wa Baraza la Wawakilishi la Marekani kwenda Taipei, mzozo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani unaendelea.

"China inapinga vikali mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na Taiwan," Shu Jueting amesema hivi punde. Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China anasema kwamba kila kitu kitafanywa "kulinda mamlaka ya China na kulinda maslahi ya China".

Shirika la habari la New China kwa mara nyingine limeishutumu Ikulu ya White House wikendi hii kwa "kucheza na moto", baada ya kuwasili Jumapili Agosti 14 kwa wabunge wa Marekani katika kisiwa hicho.

Kwa upande wake, utawala wa Marekani unatangaza "mpango kabambe wa kuhitimisha ahadi za kiwango cha juu cha biashara" msimu ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.