Pata taarifa kuu

Rais Putin adai kuwa silaha za Urusi zimetumika 'katika mazingira ya mapigano halisi'

Vladimir Putin hakuwa na maneno yenye nguvu ya kutosha kusifia silaha za Urusi kwa washirika wake wa kigeni , Jumatatu hii, Agosti 15. Rais wa Shirikisho hilo alikuwa akizungumza katika siku ya kwanza ya maonyesho ya kimataifa ya silaha katika jimbo la Moscow. Lakini mzozo wa Ukraine hadi sasa hauonekani kuwa onyesho bora kwa tasnia ya silaha ya Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kijeshi na Kiufundi la mwaka 2022 katika huko Patriot Park, nje ya Moscow, Jumatatu, Agosti 15, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kijeshi na Kiufundi la mwaka 2022 katika huko Patriot Park, nje ya Moscow, Jumatatu, Agosti 15, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

 

"Tuko tayari kupendekeza kwa washirika wetu na marafiki zetu aina ya kisasa zaidi ya silaha", alisisitiza Vladimir Putin, akibaini katikati ya vita vya Ukraine kwamba silaha hizi "karibu zote zilitumiwa mara kwa mara katika mazingira ya vita halisi".

Rais wa Urusi alithibitisha kwamba Moscow ina washirika wengi - ikisuiri kuwapata wateja watarajiwa - kutoka Amerika ya Kusini, Asia na Afrika kwa silaha hizi "zinazothaminiwa duniani kote".

Kwa nini Vladimir Putin anatetea kwa nguvu tasnia ya silaha ya Urusi? Labda kwa sababu vita vya Ukraine vinaendelea kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyofikiriwa na Moscow, na baadhi ya silaha, hasa katika suala la ulinzi wa anga, hazionekani kufanya kazi kama inavyotarajiwa.

Na hilo bila kutaja hasara kubwa - ambayo baadhi ya wachambuzi wanasema inaweza kuifanya sekta ya silaha ya Urusi isivutie. Sekta ambayo inaweza pia kuadhibiwa na vikwazo vya nchi za Magharibi; uzuiaji wa fedha, lakini pia vifaa vya kigeni visivyoweza kuingizwa.

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI), Urusi ilikuwa, kati ya mwaka 2017 na mwaka 2021, nchi ya pili kwa mauzo ya silaha duniani, ikiwa na 19% ya soko la dunia, lakini mauzo ya silaha zake yalipungua katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.