Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Singapore imetakiwa kumshtaki aliyekuwa rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu limeitaka nchi ya Singapore kumshtaki rais wa Sri Lanka aliyeondolewa madarakani Gotabaya Rajapaksa kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu yaliotekelezwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sri Lanka.

Aliyekuwa rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa
Aliyekuwa rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa AP - Eranga Jayawardena
Matangazo ya kibiashara

Rajapaksa aliondoka nchini mwake mapema mwezi huu baada ya makao yake rasimi kuvamiwa na maelfu ya waandamanaji waliokuwa wanalalamika kuhusu kudorora kwa uchumi wa taifa hilo.

Baada ya kuondoka nchini Sri Lanka, Gotabaya aliekelea nchini Maldives kwa kutumia ndege ya jeshi ambapo baadae alielekea nchini Singapore, alipotangaza kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wa rais.

Rajapaksa alikuwa waziri wa ulinzi nchini humo wakati wa mapigano yaliomalizika mwaka wa 2009 yaliongozwa na kundi Tamil lilokuwa likitaka kujitenga.

Mashirika ya kutetea haki za bindamu yaliwatuhumu wanajeshi wa serikali kwa kuwaua watu 40,000 raia wa kundi la Tamil katika kipindi cha majuma kadhaa ya mapambano.

Kundi hilo limeitaka Singapore kumkamata Gotabaya kwa kuhusika na visa vilivyokiuka mwongozo wa sheria za kidunia kuhusu binadamu.

Afisi ya mwanasheria mkuu wa Singapore imedhibitisha kupokea malalamishi hayo kutoka kwa kundi hilo japokuwa haikutoa ufanunzi zaidi.

Familia ya Rajapaksa kwa upande wake na yenyewe imeendelea kukana madai kuwa raia waliuawa wakati wa makabiliano na kundi la Tamil Tigers lilokuwa linataka kujitenga, ikikataa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa huru katika swala hilo.

Muda mfupi baada ya kuingia madarakani Novemba 2019, Rajapaksa, alitanagaza msamaha pamoja na kumuaachia huru afisa wa jeshi aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kuwaua raia wanane wa kundi la Tamil, wakiwemo watoto watatu.

Aidha Rajapaksa  ametuhumiwa kwa kuyafadhili makundi ya kutekeleza mauwaji nchini mwake akikana madai kuwa aliwateka wanahabari na baadae kuwauwa wakati akihudumu katika jeshi kati ya mwaka wa 2005 na 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.