Pata taarifa kuu
SRI LANKA-SIASA

Sri Lanka: Hali ya dharura imetangazwa kuelekea uchaguzi wa rais mpya

Kaimu rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ametangza hali nyengine ya dharura katika taifa hilo linalokumbwa na mzozo wa kiuchumi hatua hiyo ikitajwa kama njia moja ya kurejesha utulivu wakati ambapo bunge linapotarajiwa kumchagua rais mpya wiki hii.

Ranil Wickremesinghe akiapishwa kuwa kaimu wa Sri Lanka.
Ranil Wickremesinghe akiapishwa kuwa kaimu wa Sri Lanka. AP
Matangazo ya kibiashara

Wickremesinghe ameeleza kuwa hatua hii pia imechukuliwa kwa ajili ya usalama wa raia pamoja na kuwezesha usambazaji wa bidhaa muhimu kwa jamii.

Viongozi wanaokumbwa na utata nchini Sri Lanka wamekuwa wakitangaza hali ya dharura kwenye taifa hilo tangu mwezi Aprili, wakati ambapo mandamano makubwa dhidi ya serikali yalianza kushuhudiwa kulalamikia kudorora kwa yali ya uchumi pamoja na upungufu wa bidhaa muhimu kama vile dawa na mafuta.

Mapema leo Jumatatu jiji kuu la Colombo limeonekana kuwa tulivu raia wakisalia nyumbani kwa hofu ya kabiliana na walinda usalama.

Askofu Jeewantha Peiris, mmoja wa viongozi wanaopanaga mandamano nchini humo, ameeleza kuwa hali ya dharura iliyotangazwa na kaimu rais ni njia moja ya kutia uwoga waandamanaji kudai haki.

Juma lilopita, Wickremesinghe alikuwa ametangaza hali nyengine ya dharura, baada ya rais Gotabaya Rajapaksa aliyeondolewa madarakani kutoroka nchini humo kufuatia mandamano makubwa dhidi ya utawala wake.

Rajapaksa alitorokea nchini Maldives ambapo alielekea Singapore baada ya maelefu ya raia waliokuwa wanapinga utawala wake jijini Colombo kuvamia makazi yake rasimi na afisi zake.

Wickremesinghe aliyeapishwa kuhudumu kama kaimu rais siku ya Ijuma, ameahidi kufuatia sheria pamoja na kurejesha hali ya kawaida baada ya mandamano ya miezi kadhaa ya kulalamikia hali mbaya ya uchumi na ugumu wa maisha.

Bunge la taifa hilo limefanya kikao siku ya Jumamosi kupanga namana ya kumteua rais atakayehudmu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Wickremesinghe, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rajapaksa, ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuteuliwa kuhudumu kama rais. Japokuwa wanadamanaji wanamtaka kuondoka hali inayotarajiwa kuzua wasiwasi zaidi iwapo atateuliwa katika wadhifa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.