Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Sri Lanka: Rais Rajapaksa ameondoka nchini kwa kutumia ndege ya jeshi.

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameondoka nchini humo kwa kutumia usafiri wa ndege ya kijeshi, hatua inayokuja wakati huu ambapo mandamano ya kulalamikia uchumi mbaya unaokabili taifa hilo yakionekana kushika kasi.

Gotabaya Rajapaksa,rais wa Sri Lanka anayekumbwa na utata.
Gotabaya Rajapaksa,rais wa Sri Lanka anayekumbwa na utata. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Jeshi ya la anga limedhitisha kuwa rais huyo mwenye umri wa miaka 73, mkewe pamoja na walinzi wawili wametorokea katika visiwa vya Maldives.

Kuondoka kwa Rajapaksa nchini humo kunafikisha kikomo kwa utawala wa familia yake ambayo imeongoza Sri Lanka kwa miaka kadhaa.

Rais amekuwa mafichoni tangu siku ya jumamosi baada ya wandamanaji kuvamia makazi yake, rais akiahidi kujiuzulu siku ya jumatano ya tarehe 13 Julai.

Taarifa zinasema kuwa rais huyo huenda akasafiri kuelekea nchi ya tatu baada ya kuwa katika visiwa vya Maldives kwa muda.

Haya yanajiri wakati pia ambapo kakake mkubwa amabye pia aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha Basil Rajapaksa, naye pia akiripotiwa kuwa safarini kuelekea nchini Marekani.

Raia wa Sri Lanka wamendelea kuutuhumu utawala wa rais Rajapaksa kwa changamoto za kiuchumi ambazo zimekumba taifa hilo kwa miaka kadha sasa.

Kwa miezi kadhaa, raia wa taifa hilo wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa bidhaa muhimu ikiwemo petroli, chakula, dawa pamoja na kushuhudia mgao wa umeme.

Katiba ya Sri Lanka, inamkinga rais dhidi ya kushtakiwa wakati akiwa madarakani taarifa zikisema kuwa Rajapaksa alipanga kuondoka nchini humo kabla ya kutangaza kujiuzulu kama njia moja ya kumkinga dhidi ya kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.