Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Rais wa Sri Lanka Rajapaksa kuwasilisha barua ya kujiuzulu leo:Spika.

Spika wa bunge la kitaifa nchini Sri Lanka, ametanagaza kuwa rais anayekumbwa na utata Gotabaya Rajapaksa anapanga kutuma barua rasimi ya kuondoka madarakani hii leo.

Wandamanaji wakiwa katika makazi ya waziri mkuu wa Sri Lanka.
Wandamanaji wakiwa katika makazi ya waziri mkuu wa Sri Lanka. AP - Rafiq Maqbool
Matangazo ya kibiashara

Aidha spika huyo ameleza kuwa rais Rajapaksa ambaye yuko nje ya nchi amepigwa simu ambapo amefafanuliwa kuhusu nia yake ya kutaka kufanya hivyo hivi leo, awali alitarajiwa kujiuzulu siku ya jumamosi.

Barua rasimi ya kujiuzulu itatoa nafasi kwa Sri Lanka kupanga serikali mpya, rais wa muda akitarajiwa kuongoza kwa kipindi cha siku 30 kabala ya wabunge kupiga kura kumchagua kiongozi mpya.

Haya yanajiri wakati huu kituo cha pili televisheni nchini humo kikifungwa, ikiwa imepita saa moja tu baada ya kituo kingine kikubwa cha kitaifa cha Rupavahini, kusistisha opersheni zake baada ya wandamanaji kuvamia majengo yake.

Aidha polisi wametumia mambomu ya kutoa machozi kutawanaya wandamanaji ambao wamevamia makazi yake waziri mkuu Ranil Wickremesinghe.

Picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijami, zimewaonyesha wandamanaji wakipanda juu ya viti wengine wakionekana kutawala nyumbani kwa waziri mkuu kabala ya kabiliana wa walinda usalama.Awali waliwazidi nguvu maofisa wa polisi kabala ya kuingia katika makazi yake.

Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe,ambaye kwa sasa anahudumu kama rais wa muda kwa mujibu wa agizo la spika baada ya kushauriana na Rajapaksa , amewataka wanajeshi kufanya wawezavyo kurejesha utulivu.

Rajapaksa kwa sasa anasemekana kuwa yuko mafichoni katika visiwa  vya Maldives.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.