Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Sri Lanka: Wandamanji wapinga serikali inayojumuisha familia ya Rajapaksa.

Maelfu ya wandamanaji nchini Sri Lanka wameendelea kupiga kambi katika makazi ya rasimi ya rais na yale ya waziri mkuu wakiituhumu familia ya Rajapaksa kuwa sehemu kubwa ya changamoto za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.  

Wandamanji wakistarehe ndani ya makazi rasimi ya rais wa  Sri Lanka.
Wandamanji wakistarehe ndani ya makazi rasimi ya rais wa Sri Lanka. REUTERS - DINUKA LIYANAWATTE
Matangazo ya kibiashara

Machafuko yaliaanza siku ya jumamosi wakati ambapo raia wenye ghadhabu walivamia makazi rasimi ya rais Gotabaya Rajapaksa, mwenye umri wa miaka 73, anyetokea katika uko wa Rajapaksa ambaye waandamanji wanamtuhumu kwa misukusuko ya kiuchumi inayoshuhudiwa nchini humo tangu mwaka wa 1948.

Rajapaksa anatarajiwa kujiuzulu rasimi siku ya jumatano .Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe naye pia akiashiria kuwa yuko tayari kuondoka ofisini baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja inayojumisha vyama vyote vya kisiasa, serikali ambayo itapewa jukumu la kuiondoa Sri Lanka katika changamoto zilizopo.

Wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja umepingwa vikali na wandamanaji ambao wamesema  hatawaondoka katika majumba ya serikali hadi pale ambapo rais na waziri mkuu watajiuzulu rasimi kutoka kwa nyadhifa zao.

Baadhi ya wandamanaji hawataki chama the Sri Lanka Podujana Party (SLPP) kinachotawaliwa na familia ya Rajapaksa kuwa sehemu ya serikali ya umoja.

Katiba ya Sri Lanka inaweka wazi kuwa iwapo rais na waziri mkuu wataondoka ofisini, spika wa bunge atachukua nafasi ya rais. Kinaya ni kwamba spika wa sasa Mahinda Yapa Abeywardene anatokea katika familia ya Rajapaksa.

Tangu mawaka wa 1978, Sri Lanka imekuwa chini ya mfumo unaompa rais madaraka makubwa kabla ya mfumo huo kufanyiwa marekebisho mwaka wa 2015 bunge likipewa baadhi ya mamlaka.

Mwezi oktoba mwaka wa 2020, mwaka moja baada ya kuwa madarakani kama rais, Gotabaya Rajapaksa, kwa usaidizi wa kakake mkubwa, wakati huo akihudumu kama waziri mkuu Mahinda Rajapaksa, waliwasilisha muswada bungeni uliomrejeshea madaraka makubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.