Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Sri Lanka: Mmoja wa familia ya Rajapaksa amezuiwa kuondoka nchini humo.

Maofisa katika idara ya uhamiaji nchini Sri Lanka, wanasema kuwa wamemzuia kakake rais wa taifa hilo na aliyekuwa waziri wa fedha wa zamani Basil Rajapaksa kutoondoka nchini humo.

Machafuko dhidi ya utawala wa rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa.
Machafuko dhidi ya utawala wa rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa. REUTERS - DINUKA LIYANAWATTE
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kuzuiwa kwa waziri huyo wa zamani inakuja wakati huu shinikizo zinapoendelea kutolewa kwa familia ya Rajapaksa kwa kutumbukiza Sri Lanka katika mzozo wa kiuchumi.

Haijabainika ni wapi Rajapaksa, ambaye ana uria wa Marekani alikuwa amekusudia kuelekea.

Alijiuzulu kutoka kwa wadhifa wa waziri wa fedha mapmea mwezi aprili kutokana na ongezeko la maandamano ya kulalamikia ukosefu wa mafuta, chakula na bidhaa nyengine muhimu swala lilomlazimu pia kujiuzulu kutoka nafasi yake katika bunge mwezi Juni.

Haya yanajiri wakati huu ambapo pia kaka yake mkubwa Gotabaya Rajapaksa, akitarajiwa kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wa urais siku ya jumatano kama njia moja ya kutoa nafasi ya uundwaji wa serikali ya umoja.

Hatua ya kujiuzulu kwa rais Gotabaya Rajapaksa, imekuja baada ya waaandamanji wenye ghadhabu kuvamia makazi yake rasimi jumamosi ya wiki iliyopita wakitaka aondoke madarakani.

Rais Gotabaya hajaonekana katika umma tangu siku ya Ijuma na haijabainika wazi ni wapi aliko.

Picha za Basil Rajapaksa akiwa katika eneo la kusubiri kusafiri zimesambazwa na vyombo vya habari nchini humo katika mitandao ya kijamii, raia wakionekana kukasirishwa na hatua yake ya kutaka kuondoka nchini Sri Lanka.

Familia ya Rajapaksa, akiwemo waziri mkuu wa zamani Mahinda Rajapaksa, imetawala siasa za taifa hilo lenye idadi ya watu milioni 22 kwa miaka kadhaa idadi kubwa ya raia nchini humo wakiituhumu familia hiyo kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayowakumba kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.