Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Sri Lanka: Mamilioni ya pesa iliyopatikana katika makazi ya Rajapaksa imechukuliwa na polisi.

Polisi nchini Sri Lanka, imesema kuwa imewasilisha Millioni ya pesa iliyopatikana katika makazi ya rais wa taifa hilo Gotabaya Rajapaksa baada yake kutoroka  makazi yake siku ya jumatatu.

Waandamanji wakiwa katika makazi ya rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa.
Waandamanji wakiwa katika makazi ya rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa. REUTERS - DINUKA LIYANAWATTE
Matangazo ya kibiashara

Waandamanji walipata shillingi milioni 17.85 pesa za Sri Lanka baada ya kuvamia makazi ya rais huyo siku ya jumamosi na baadae kuziwasilisha kwa maofisa wa polisi nchini humo.

Aidha maofisa katika taifa hilo wameeleza kuwa stakabadhi zengine zilipatikana katika makazi hayo zikiwa zimehifadhiwa katika masanduku.

Rajapaksa, amekuwa akitumia makazi hayo baada ya waandamanji kumfurusha katika makazi yake ya kibanafsi machi 31.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 aliondolewa katika jengo hilo kupitia mlango wa nyuma kwa usaidizi wa maofisa wa usalama.

Hadi Jumatatu ya leo, haikuwa inajulikana yuko wapi rais Rajapaksa japokuwa waziri mkuu Ranil Wickremesinghe akieleza kuwa Rajapaksa alifahamisha kuhusu mpango wake wa kujiuzulu.

Wickremesinghe mwenye umri wa miaka 73, kwa sasa atahudumu kama rais wa muda japokuwa ameleza nia yake ya kuachia nafasi hiyo iwapo makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja yataafikiwa.

Rajapaksa, awali alikuwa amemueleza spika wa bunge la kitaifa Mahinda Abeywardana kwamba atajiuzulu siku ya jumatano kama njia moja ya kutoa nafasi ya ubadilishanaji wa madaraka kwa amani, saa chache baada ya kutimuliwa katika makazi yake rasimi.

Maelfu ya waandamanji waliteka makazi yake Rajapaksa yalioko kando ya bahari muda mfupi baada yao kushambulia makazi yake rasimi.

Waandamanji wamekuwa wakipiga kambi nje ya makazi rasimi ya rais kwa zaidi ya miezi mitatu wakitaka ajiuzulu kutokana na hali mbaya ya uchumi inayolikabili Sri Lanka.

Rajapaksa, anatuhumiwa kwa utawala mbaya, hali ambao imelitumbukiza taifa lake lenye zaidi ya watu milioni 22 katika ugumu wa maisha.

Waandamanji aidha wanamataka Wickremesinghe, mwanasiasa wa upinzani aliyeteuliwa waziri mkuu mwezi mei kwa minajili ya kujaribu kuinusuru Sri Lanka kutoka katika mzozo wa kiuchumi naye pia kujiuzulu

Sri Lanka, ilishindwa kulipa deni lake la dolla za marekani bilioni 51 mwezi Aprili na kwa sasa imo katika mazunguzmo na shirika la fedha duniani IMF kutafuta mbinu ya kulipa deni hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.