Pata taarifa kuu

Korea Kusini: Seoul na Washington zazindua makombora ya masafa marefu

Korea Kusini na Marekani zimerusha makombora manane ya masafa marefu leoJumatatu Juni 6, kujibu jaribio kama hilo la Korea Kaskazini jana Jumapili, jeshi la Korea Kusini limesema.

Chombo kikubwa cha Marejkani kinachobeba ndege "USS Ronald Reagan" katikati ya kikosi cha wanamaji cha Marekani na Korea Kusini, Juni 4, 2022.
Chombo kikubwa cha Marejkani kinachobeba ndege "USS Ronald Reagan" katikati ya kikosi cha wanamaji cha Marekani na Korea Kusini, Juni 4, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili lililodumu dakika kumi, lililozinduliwa na washirika wa Korea Kusini na Marekani, ilnakuja siku moja baada ya Pyongyang kurusha makombora manane ya masafa mafupi, kufuatia mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani ambapo chombo kikubwa cha Marekani kinachobeba ndege kinachopima uzito wa tani 100,000, USS Ronald Reagan kimeshiriki. Wakuu wa majeshi kutoka nchi hizi wamesema washirika walirusha kombora la Mfumo wa Mbinu wa Kijeshi wa Kombora (ATACMS) alfajiri ya Jumatatu dhidiya maeneo yanayopatikana katika Bahari ya Mashariki, ambayo pia inaitwa Bahari ya Japan.

Jaribio jingine la nyuklia?

"Jeshi letu linalaani vikali uchokozi wa makombora ya masafa marefu unaofanywa na Korea Kaskazini na kuitaka kusitisha mara moja vitendo vinavyoongeza mvutano wa kijeshi kwenye rasi hiyo ya Kora," jeshi la Korea Kusini limeongeza katika taarifa yake. Pyongyang imeongeza juhudi mwaka huu kuboresha mpango wake wa silaha, licha ya vikwazo vikali vya kiuchumi. Maafisa na wachambuzi wameonya kuwa utawala wa Kim Jong-un unajiandaa kufanya jaribio jingine la nyuklia.

Jaribio la pili lenye nguvu

Tukio hili la Jumatatu ni onyesho la pili la nguvu la pamoja la washirika chini ya Rais mpya wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol, ambaye ameapa kuimarisha msimamo wake katika kukabiliana na chokochoko za Pyongyang. "Serikali yetu itajibu kwa uthabiti na kwa ukali uchochezi wowote unaofanywa na Korea Kaskazini," Yoon amesema katika hotuba yake wakati wa siku ya kumbukumbu siku ya Jumatatu. Mwezi uliopita, Seoul na Washington zimefanya jaribio lao la pamoja, hatua yao ya kwanza ya pamoja tangu mwaka 2017, baada ya Pyongyang kurusha makombora matatu ya masafa mafupui, likiwemo moja linaloaminika kuwa la masafa marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.