Pata taarifa kuu

Sri Lanka: Hotuba ya Gotabaya Rajapaksa yakashifiwa na raia .

Raia nchini Sri Lanka, wameikashifu hotuba ya rais Gotabaya Rajapaksa ya usiku wa kuamkia alhamis ya Mei 12 ambapo alikwepa kuzungumzia wito wa raia wa kumtaka kujiuuzulu akiahidi kurejesha utaratibu kwenye taifa hilo.

Wanajeshi nchini Sri Lanka wakipiga doria.
Wanajeshi nchini Sri Lanka wakipiga doria. © REUTERS/Dinuka Liyanawatte
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake ya kwanza kwa umma tangu mchafuko kuaanza kushuhudiwa nchini mwaka mwezi jana, ameeleza kuwa atagawa baadhi ya mamlaka yake kwa bunge japokuwa hakutaja ni lini hilo litatekelezwa.

Raia nchini Sri Lanka, wameendelea kusisitiza kuwa ni lazima rais huyo aondoke madarakani kutokana na kushindwa kutoa suluhu ya mzozo wa kiuchumi unaolikumba taifa lake, idadi kubwa ya raia hao ikisema hotuba yake haikuzungumzia baadhi ya maswala muhimu kwao.

Maelfu ya watu nchini humo wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile twitter wamemtaka rais Gotabaya kuiga mfano wa waziri mkuu Mahinda Rajapaksa ambaye tayari amejiuzulu juma hili.

Mahinda Rajapaksa ni kakake rais Gotabaya Rajapaksa aliyejiuzulu kutokana na shinikizo za waandamanji nchini humo wanaotoka familia ya Gotabaya yote kuondoka madarakani.

Siku ya jumatatu ya wiki hii, maandamano ya majuma kadhaa ya amani kwenye taifa hilo yaligeuka kuwa ghasia baada ya wafuasi wa Mahinda Rajapaksa kuwashambulia waandamanji wanaoipinga serikali waliokuwa wamekusanyika kuendeleza shinikizo zao kwa serikali kujiuzulu.

Maofisa wa usalama nchini Sri Lanka wameamurishwa kuwapiga risasi waandamanji wanaotumia wakati huu wa maandamano kuharibu mali, baadhi yao wakionekana kulenga mali inayomilikiwa na familia ya Gotabaya.

Makataa ya watu kutembea nje nyakati za usiku pamoja na agizo la kufungwa kwa maduka, sehemu za biashara na maofisi yamesisitishwa kwa muda ila yanatarajiwa kurejeshwa alhamis mchana.

Raia wanalalamikia ukosefu wa bidhaa muhimu kama vile chakula na mafuta ambavyo havipatikana na iwapo vitapatikana bei yake ni ghali.

Rais Gotabaya Rajapaksa, anatarajiwa kumtaja waziri wake mkuu mpya kama njia moja ya kujaribu kuliondoa taifa hilo kutoka kwa mzozo wa kiuchumi ambao umesababisha maandamano ya raia wanaotaka mabadiliko kufanyika.

Sri Lanka ina idadi ya watu milioni 22 ambao wanapitia kipindi kigumu zaidi kuwahi onekana nchini humo tangu uhuru wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.