Pata taarifa kuu

Mwanahabari wa Al Jazeera ameuawa na wanajeshi wa Israeli katika eneo la West Bank

Shireen Abu Aqleh ,  Mwanahabari maarufu wa shirika la habari la Al Jazeera , ameuawa baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israeli wakati akifuatilia tukio la shambulio katika kambi ya wakimbizi ya  Jenin  katika eneo la West Bank, imesema taarifa ya shirika hilo.

Wanahabari wakiubeba mwili wa  Shireen Abu Aqleh mwanahabari wa Al Jazeera.
Wanahabari wakiubeba mwili wa Shireen Abu Aqleh mwanahabari wa Al Jazeera. AFP - JAAFAR ASHTIYEH
Matangazo ya kibiashara

Al Jazeera inaeleza kuwa mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 51 ameuawa kimaskusudi na vikosi vya Israeli madai amabyo jeshi hilo limejitenga nayo.

Vikosi vya Israeli japokuwa vimekiri kutekeleza operesheni kwenye kambi hiyo ambayo ni ngome kubwa ya wapiganaji wa palestina kaskazini mwa West Bank, vimekana madai kuwa vinawalenga wanahabari.

Aidha jeshi limedhibitisha uwepo wa makabiliano makali kati ya maofisa wake na washukiwa ambapo limesema limeanzisha uchunguzi katika tukio hilo ambalo limeeleza kuwa kuna uwezekano wanahabari walipigiwa risasi na raia wa palestina waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

 

00:27

Linda Thomas-Greenfield Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa

Mpiga picha wa shirika la habari la AFP, aliyekuwepo wakati wa tukio hilo ameeleza kuwa Abu Aqleh alikuwa amevalia mavazi yaliokuwa yanamtambulisha kama mwanahabari kabla ya kupigwa risasi.

Tayari Al Jazeera, imetaka jamii ya kimataifa kuiwajibisha Israeli kwa kumlenga na kumuuwa kimakusudi Abu Aqleh.

Mwanahabari mwengine wa Al Jazeera ,Ali Al-Samudi,ambaye ni mzalishaji wa vipindi naye pia amejeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.

Mamlaka nchini palestina nazo pia zimekashifu na kulaani mauwaji ya Abu Aqleh ikisema kuwa mauawaji hayo ni njia moja ya Israeli kutaka kuficha ukweli kuhusu hatua yake ya kuendelea kusalia katika eneo la West Bank, kundi la kiisilamu la Hamas linalotawala eneo la Gaza limetaja mauaji ya mwanahabari huyo kama swala ambalo halikutafakariwa.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Israel imetangaza kufanya uchunguzi kubaini kilichotekea kwa ushirikiano na mamlaka nchini palestina, Qtar imelaani mauwaji hayo, balozi wa Israel nchini Marekani naye ametaka uchunguzi kufanyika kubaini kilichotokea akieleza kusikitsihwa na hali hiyo.

Waziri mkuu wa Israeli, Naftali Bennett , katika taarifa yake ameeleza kuwa kuna uwezekano mwanhabari huyo wa Al Jazeera  Shireen Abu Aqleh aliuwawa na Palestina. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.