Pata taarifa kuu

Indonesia yamwalika Putin kwenye mkutano wa G20

Tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, nchi za Magharibi zimekuwa zikitafuta kuitenga Urusi katika ukumbi wa kimataifa. Lakini nchi kadha zinataka kudumisha msimamo wa kutoegemea upande wowote dhidi ya Moscow. Na sasa Rais wa Indonesia amemwalika Vladimir Putin kushiriki katika mkutano wa nchi zinazoongoza kiuchumi duniani, G20, utakaofanyika mwezi Novemba katika kisiwa cha Bali.

Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Kremlin, Jumatatu Aprili 18, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Kremlin, Jumatatu Aprili 18, 2022. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Indonesia Joko Widodo alitangaza Ijumaa kwamba amemwalika mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kuthibitisha kuwa amemwalika Rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye mkutano wa G20 uliopangwa kufanyika Novemba nchini Indonesia.

"Nimemwalika Rais Zelensky kushiriki katika mkutano wa G20," alisema kiongozi wa Indonesia, akipendekeza kwamba maelewano yamepatikana kwa mkutano uliopangwa kufanyika Bali, wakati wanachama wa kundi hilo wamegawanyika sana tangu mwanzo ."Hatuwezi kujifanya kuwa hakuna kilichotokea," Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Ijumaa. Hakuna jibu, hata hivyo lililotolewa, kwa swali la mwandishi wa habari kuhusu kama Joe Biden atakataa kushiriki kwenye mkutano wa G20. Hali ya utawala wa Marekani kwa kweli si rahisi: baada ya kumwita Vladimir Putin mhalifu wa vita na kuishutumu Urusi kwa mauaji ya halaiki nchini Ukraine, inawezekanaje kufikiria kukutana na rais wa Urusi katika mkutano huo wa nchi zilizostawi kiuchumi duniani?

Ikulu ya White House ina msimamo wake: kufukuzwa kwa Urusi katika kundi la G20 haiwezekani kwa kukukosekana kwa maelewano. Katika mkutano wa mawaziri wa fedha wa G20 mwezi Aprili, ujumbe wa Marekani na washirika kadhaa walisusia baadhi ya vikao kupinga ushiriki wa Urusi. Je, Marekani inaweza kuamua kutuma wajumbe wa ngazi ya chini huko Bali? Kutokuwepo kwa Joe Biden kutatoa nafasi kwa Urusi na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.