Pata taarifa kuu

Urusi yainyooshea kidole cha lawama Marekani kuhusu mzozo kati yake na Ukraine

Urusi inasema, Marekani haishughulikii sharti lake la kiusalama kuhusu mzozo wa Ukraine, lakini inaacha nafasi ya kuendelea kwa mazungumzo ili kutuliza hali ya wasiwasi inayoshuhudiwa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Desemba 21, 2021 huko Moscow.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, Desemba 21, 2021 huko Moscow. AP - Sergey Guneyev
Matangazo ya kibiashara

Marekani na mataifa ya Magharibi, yameendelea kuishtumu Urusi kwa kuwa na mpango wa kuishambulia jirani yake Ukraine, madai ambayo inaendelea kukanusha.

Waziri wa Mambo nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, wako tayari kwa mazungumzo na Urusi, lakini pia kujilinda iwapo nchi yao itavamiwa.

Kwa upande mwingine Marekani nayo imekataa sharti la  Urusi kuhusu kuzuiwa kwa Ukraine kuwa mwanachama wa jeshi la umoja la kujihami kwa nchi ya Magharibi NATO.

Marekani imesisitiza kutumia njia za kidiplomasia, licha ya kuonesha kukataa kila pendekezo lililotolewa na Urusi kuhusu Ukraine.

Wakati huo huo Ujerumani imeapa kuchukua hatua kali iwapo Urusi itaivamia Ukraine, huku vikwazo vikitarajiwa katika mradi wenye utata wa bomba la gesi unaogharamiwa na Urusi na Ujerumani unaojulikana kama Nord Stream 2. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock leo ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa wanashughulikia vikwazo vikali na washirika wao wa Magharibi na vitajumuisha masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na mradi wa Nord Stream 2.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.