Pata taarifa kuu

Bingwa wa mchezo wa Tennis duniani Novak Djokovic azuiwa kuingia Australia

Serikali ya Australia imefuta kibali cha kuingia nchini humo cha bingwa wa mchezo wa Tennis duniani Mserbia Novak Djokovic, kufuatilia kile ambacho maafisa nchini humo wanasema mchezaji huyo hakutimiza masharti ya kuingia nchini humo.

Bingwa wa mchezo wa Tennis duniani Serbia, Novak Djokovic,  wakati wa fainali ya Australian Open mjini Melbourne Februari 21, 2021.
Bingwa wa mchezo wa Tennis duniani Serbia, Novak Djokovic, wakati wa fainali ya Australian Open mjini Melbourne Februari 21, 2021. William WEST AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja baada ya mchezaji huyo kusema amepata msamaha wa kuingia nchini Australia kushiriki kwenye michezo ya Australia Open kuanzia Januari 17 bila ya kuwa na cheti cha kuonesha kuwa amepata chanjo.

Waziri Mkuu Scott Morrison amesema sheria lazima ziheshimiwe.

Djokovic hata hivyo hajazungumzia lolote kuhusu iwapo amechanjwa, ila mwaka uliopita, alisema alikuwa haungi mkono chanjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.