Pata taarifa kuu

Mkutano kati Biden na Erdogan kufanyika Roma Jumapili hii kando ya mkutano wa G20

Rais wa Marekani Joe Biden atakutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye nchi yake ni mwanachama wa NATO, Jumapili mjini Roma kando ya mkutano wa nchi zilizostawi kiviwanda na zinazoendelea kiuchumi, G20, kulingana na afisa wa Marekani.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atakutana na Joe Biden kwa mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana mjini Brussels siku ya Jumatatu.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atakutana na Joe Biden kwa mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana mjini Brussels siku ya Jumatatu. Adem ALTAN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja wakati kunaripotiwa mvutano kati ya Uturuki na Marekani, hasa kutokana na Ankara kununua mfumo wa ulinzi wa Urusi.

Lakini Rais Erdogan ameachana na hatua yake ya kuwafukuza mabalozi kumi wa nchi za Magharibi, akiwemo balozi wa Marekani, ambao walioomba kuachiliwa kwa kiongozi mmoja wa asasi za kijamii mzaliwa wa Paris, Osman Kavala, anayefungwa jela kwa miaka minne bila kesi.

Siku ya Jumamosi (Oktoba 23), Erdogan alimuelezea Kavala kama "wakala" wa bilionea wa Kimarekani aliyezaliwa Hungary, George Soros, ambaye amekuwa akiandamwa mara kwa mara na wanasiasa wa mrengo wa kulia na wenye nadharia za hujuma dhidi ya Mayahudi.

Kesi dhidi ya Kavala

Kavala, mwenye umri wa miaka 64, amekuwa kizuizini tangu mwaka 2017 bila ya kutiwa hatiani kwenye mashitaka yanayomuhusisha na maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2013 na jaribio la mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa mwaka 2016.

Mabalozi wa mataifa ya Magharibi walikuwa wametowa wito wa kesi yake "kuendesha kwa haki na kwa haraka."

Wafuasi wa Kavala wanamuona kama ya msako wa jumla jamala unaofanywa na Erdogan baada ya kunusurika kwenye jaribio la mapinduzi la mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.