BANGLADESH-USALAMA
Bangladesh: Saba wauawa kwa kupigwa risasi katika kambi ya wakimbizi ya Rohingya
Washambuliaji wamewauwa watu wasiopungua saba Ijumaa katika shambulio kwenye seminari ya Kiislamu katika kambi ya wakimbizi ya Rohingya nchini Bangladesh, mpakani na Burma, polisi wamesema.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Baadhi ya wahanga waliuawa kwa kupigwa risasi, wengine walidungwa visu, mkuu wa polisi wa eneo hilo almeliambia shirika la habari la AFP.
Mauaji hayo yanajiri wakati mivutano ikiongezeka baada ya mauaji ya kiongozi wa Rohingya katika kambi moja wiki tatu zilizopita.