Pata taarifa kuu
JAPAN-SIASA

Fumio Kishida achaguliwa Waziri Mkuu wa Japani

Baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa chama tawala Jumatano, Fumio Kishida, 64, amehaguliwa kuwa waziri mkuu Jumatatu hii na bunge la Japan.

Fumio Kishida alishinda kura 311 katika Baraza la wawakilishi dhidi ya kura 124 za kiongozi mkuu wa upinzani, Yukio Edano. Katika Bune la Seneti alipata kura 141, dhidi ya 65 za Yukio Edano.
Fumio Kishida alishinda kura 311 katika Baraza la wawakilishi dhidi ya kura 124 za kiongozi mkuu wa upinzani, Yukio Edano. Katika Bune la Seneti alipata kura 141, dhidi ya 65 za Yukio Edano. REUTERS - KIM KYUNG-HOON
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu mpya nchini Japani, Fumio Kishida, 64, amechaguliwa Jumatatu, Oktoba 4, na Bunge na anatarajiwa kutangaza timu yake ya serikali baadaye, baada ya uchaguzi wake Jumatano iliyopita kuwa rais wa chama tawala.

Fumio Kishida alishinda kura 311 katika Baraza la wawakilishi dhidi ya kura 124 za kiongozi mkuu wa upinzani, Yukio Edano. Katika Bune la Seneti alipata kura 141, dhidi ya 65 za Yukio Edano.

Serikali inayomaliza muda wake ikiongozwa na Yoshihide Suga, 72, ilijiuzulu leo asubuhi. Yoshihide Suga anaondoka madarakani baada ya kuhudumu mwaka mmoja, akislazimika kuachia ngazi baada ya kupoteza imani kwa raia kwa sababu ya kutokana na usimamizi wake mbaya katika kukabiliana mgogoro wa kiafya na kushikilia Michezo ya Olimpiki kufanyika Tokyo kwa gharama zote msimu huu wa joto.

Fumio Kishida atakuwa na kibarua kigumu kasa kuinua uchumi wa Japani, huku akitakiwa kuepuka kuibuka tena kwa mgogoro wa kiafya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.