Pata taarifa kuu
JAPAN-SIASA

Japani: Fumio Kishida kuchukua mikoba ya Yoshihide Suga

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Japana, Fumio Kishida, amechaguliwa Jumatano hii Septemba 29 kuwa mwenyekiti wa chama tawala, na kumshinda Taro Kono kutoka mrengo wa kulia.

Katika hotuba yake, Kishida ameapa kukiongoza chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika katika kipindi cha wiki chache na kuendelea kupambana na janga la Covid-19 ambalo limeuathiri pakubwa uchumi wa Japan.
Katika hotuba yake, Kishida ameapa kukiongoza chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika katika kipindi cha wiki chache na kuendelea kupambana na janga la Covid-19 ambalo limeuathiri pakubwa uchumi wa Japan. AP - Du Xiaoyi
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa zamani wa mambo ya nje Fumio Kishida, 64, amechaguliwa kuwa mkuu wa chama tawala nchini Japan Jumatano na atakuwa waziri mkuu wa nchi hiyo wiki ijayo.

Fumio Kishida, anayechukuliwa kuwa na msimamo wa wastani, ameibuka mshindi wakati wa pambano la mwisho la kuwania kiti ha uenyekiti wa chama cha Liberal Democratic Party (PLD) dhidi ya mpinzani wake ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi, Taro Kono, 58.

Katika hotuba yake Kishida ameapa kukiongoza chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika katika kipindi cha wiki chache na kuendelea kupambana na janga la Covid-19 ambalo limeuathiri pakubwa uchumi wa Japan. Lakini Kishida hana uungwaji mkono mkubwa wa umma na ushindi wake huenda ukakiletea matatizo chama cha LDP katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 28.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.