Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Kesi ya nyambizi: Biden na Macron waahidi kurejesha 'imani' kati ya nchi zao

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Marekani Joe Biden wameahidi Jumatano Septemba 22, wakati mazungumzo ya simu, kurejesha imani kati ya Ufaransa na Marekani baada ya kuzuka mgogoro kuhusu nyambizi za Australia, ambao ungeweza kuepukwa na "mashauriano ya wazi" hapo awali, kulingana na taarifa ya pamoja kutoka Ikulu za Elysee na White House.

Emmanuel Macron na Joe Biden, Juni 12, 2021 wakati wa mkutano wa nchi mbili.
Emmanuel Macron na Joe Biden, Juni 12, 2021 wakati wa mkutano wa nchi mbili. REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

"Mashauriano ya wazi kati ya washirika juu ya maswali ya maslahi ya kimkakati kwa Ufaransa na washirika wa Ulaya yangefanya iwezekane kuepusha hali hii. Rais Biden ameahidi kutafutia ufumbuzi swala hili, ”imesema taarifa hiyo.

Wakuu hawa wawili wa Marekani na Ufaransa, ambao watakutana "Ulaya mwishoni mwa mwezi Oktoba", "wameamua kuzindua mchakato wa mashauriano ya kina yenye lengo la kuweka masharti ya kuhakikisha imani yarejea kati ya nchi zao na kupendekeza hatua madhubuti kufikia malengo ya pamoja ”.

Katika muktadha huu wa maelewano, balozi wa Ufaransa nchini Marekani, Philippe Etienne, atarudi Washington "wiki ijayo", Emmanuel Macron ameamua.

"Umuhimu wa kimkakati"

Paris ilitangaza Ijumaa kuwarejesha nyumbani mabalozi wake nchini Marekani na Australia, uamuzi ambao haujawahi kutokea dhidi ya washirika hawa wawili wa kihistoria, baada ya Canberra kuvunja kwa mkataba mkubwa wa nyambizi za Ufaransa.

Joe Biden pia amebaini kwamba ilikuwa "muhimu kwa ulinzi wa Ulaya kuwa na nguvu na ufanisi zaidi" kuchangia usalama wa bahari ya Atlantic na kukamilisha "jukumu la NATO".

Marekani "imebaini tena kuwa ushiriki wa Ufaransa na Umoja wa Ulaya katika eneo la Indo-Pacific ni wa umuhimu kimkakati," iliongeza taarifa hiyo, iliyotolewa siku sita baada ya kuzuka kwa mzozo mbaya zaidi wa kidiplomasia kati ya Marekani na Ufaransa tangu Ufaransa "kupinga" kushirika katika vita vya Iraq mnamo 2003.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.