Pata taarifa kuu
MAKEDONIA

Kumi na nne waangamia katika mkasa wa Moto Makedonia Kaskazini

Mamlaka nchini Makedonia Kaskazini imeahidi kutoa mwanga juu ya chimbuko la mlipuko uliofuatiwa na moto mkali ulioteketeza majengo ya kitengo cha Covid-19 katika jimbo dogo la Balkan, na kuua watu wasiopungua 14.

Skopje, mji mkuu wa Makedonia Kaskazini.
Skopje, mji mkuu wa Makedonia Kaskazini. Céline Develay-Mazurelle/RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Zoran Zaev ametaja tukio hilo kama "mkasa mkubwa" wakati akielekea mji mdogo wa Tetovo, kaskazini magharibi, baada ya janga hilo wakati Jamhuri ya Yugoslavia ya zamani inasherehekea miaka 30 ya uhuru wake.

"Mlipuko ulisababisha moto. Moto ulizimwa lakini watu wengi walifariki dunia," kiongozi wa serikali amesema kwenye Facebook, akiahidi kutoa mawanaga kuhusu mkasa huo. "Taasisi za mahakama zimnazuru eneo la tukio".

Ofisi ya mashtaka ya nchi hii ndogo masikini ya Balkan, yenye huduma dhaifu za afya imetangaza kwamba imeagiza uchunguzi wa miili ya watu 14 waliokufa, na kuongeza kuwa kwa baadhi ya wahanga, vipimo vya damu (DNA) vinahitajika kwa kuitambua zaidi.

"Tunachunguza ili kujua ikiwa kuna vifo vingine", ofisi ya mashtaka katika taarifa, ikibainisha hata hivyo "kwamba hakuna mhudumu wa afya hata moja ambaye amejeruhiwa au kufariki dunia".

Moto ulitokea katika kitengo kipya cha Covid-19 cha kituo cha hospitali ya Tetovo, muda mfupi baada ya kufanyika kwa maadhimisho ya uhuru wa Makedonia Kaskazini huko Skopje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.