Pata taarifa kuu
MYANMAR

Myanmar: Kundi moja la waasi ladhibiti kambi ya jeshi, hofu yatanda

Moja ya makundi makuu ya waasi nchini Myanmar, yanayokabiliana vikali na utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya kieshi nchini humo, yamedhibiti kambi ya jeshi leo Jumanne, hali ambayo inatia hofu ya kuzuka kwa makabiliano mapya na jeshi.

Mvutano kati ya wanajeshi na baadhi ya makabila mengi nchini Myanmar umeongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'a mamlakani Aung San Suu Kyi tarehe 1 Februari.
Mvutano kati ya wanajeshi na baadhi ya makabila mengi nchini Myanmar umeongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'a mamlakani Aung San Suu Kyi tarehe 1 Februari. Soe Than WIN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mvutano kati ya wanajeshi na baadhi ya makabila mengi nchini Myanmar umeongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'a mamlakani Aung San Suu Kyi tarehe 1 Februari.

Jumanne alfajiri, "askari wetu wamedhibiti kambi ya jeshi" ilioko katika jimbo la Karen (Kusini Mashariki), Padoh Saw Taw Nee, mmoja wa maafisa wa kundi la waasi la KNU ameliambia shirika la habarila AFP. Hakusema ikiwa kuna majeruhi wowote au vifo vilivyotokea baada ya kudhbiti kambi hiyo.

Uongozi wa kijeshi waapa wajiandaa kulitimua kundi la KNU

Msemaji wa utawala wa kijeshi Zaw Min Tun amethibitisha shambulio hilo, akisema "hatua zitachukuliwa" dhidi ya kundi la KNU kufuatia shambulio hilo.

Mwishoni mwa mwezi Machi, kundi hilo lilifanya uvamizi dhidi ya kambi ya jeshi na kuua wanajeshi 10.

Kuanzia mwaka 2015, jeshi lilikuwa limefikia makubaliano ya kitaifa ya kusitisha mapigano (ANC) na makundi kumi ya waasi, ikiwa ni pamoja na kundi la KNU. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.